- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamiringi Macha amewaasa wanafunzi wa Shule ya Wasichana Shinyanga Sekondari kuweka jitihada na nguvu zote katika masomo ili kuhakikisha wanafanya vizuri na baadae waweze kutimiza ndoto na malengo waliyojiwekea ukizingatia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha kila kitu ikiwemo kuleta walimu, kuweka miundombinu mbalimbali na vingine vingi iliyobakia ni ninyi kusoma kwa bidii na ndiyo shukrani zenu pekee kwake Mhe. Rais.
Ameyazungumza haya leo tarehe 18 Septemba 2024 alipotembelea shuleni hii akiwa ameambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko, Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga ndg. Said Kitinga, Mkurugenzi wa Manispaa Mwl. Alexius Kagunze na watalaam wengine.
Pamoja na ushauri huu, Mhe. Macha ameipongeza sana Manispaa ya Shinyanga kwa usimamizi wa ujenzi wa shule hii ambayo inatajwa kuwa ya mfano kutokana na ubora, thamani yake pamoja na ushirikiano wao mzuri jambo ambalo linapelekea kukamilika kwa ujenzi huu ifikapo mwishoni mwa Septemba 2024.
“Ninawataka na kuwatia moyo sana ninyi wanafunzi wote katika shule hii, muelekeze bidii na jitihada zenu kubwa katika masomo yenu ili muhakikishe kwamba mnafanya vizuri na mnakuwa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wengine ambao watafuata baada yenu na pia kwa wanafunzi wa shule zingine na hatimaye muweze kuzifikia, kutimiza na kuziishi ndoto zenu pamoja na malengo mliyojiwekea ukizingatia Mhe. Rais wetu mpendwa amekwishaleta na kuwezesha kila kitu hapa” amesema RC Macha.
Akipokea ushauri Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze ameahidi kutekeleza kazi kwa viwango na kwa wakati ili kwenda na muda uliokusudiwa ambapo ujenzi wa shule hii unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Septemba 2024.
Aidha Mwl. Kagunze ameongeza kuwa kufikia Januari 2025 Shule ya Wasichana Shinyanga Sekondari itakuwa tayari kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao watakuwa wamechaguliwa hapa kwakuwa mindombinu yote ya shule ipo tayari.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga