- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameipongeza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa Halmashauri ya kwanza kutoa mikopo ya asilimia kumi kwa mkoa wa Shinyanga tangu mikopo hiyo iliporejeshwa ili kuvinufaisha vikundi vya Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu Kwa vikundi vilivyoomba pamoja na usimamizi mzuri na usafi wa mazingira.
RC macha ametoa pongezi hizi leo Januari 9,2025 alipokutana na kufanya kikao kazi na watumishi wa serikali na taasisi za umma zilizopo ndani ya mkoa wa Shinyanga, kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa wa shinyanga.
“Manispaa ya Shinyanga ndiyo halmashauri pekee kwa mkoa wa Shinyanga iliyoanza kutekeleza kikamili na kwa haraka agizo la serikali kutoa mikopo ya asilimia kumi kwa mkoa huu kwa vikundi vya vijana , wanawake na watu wenye ulemavu tangu serikali iliporejesha mikopo hii, lengo la serikali ni kuwasaidia wananchi kuondokana na umasikini kupitia mikopo hii, niziagize Halmashauri zote zilizopo ndani ya mkoa huu nendeni mkaweke utaratibu mzuri ili vikundi hivyo viweze kupata mikopo hiyo pamoja na kusimamia vizuri utunzaji na usafi wa mazingira kama ilivyo manispaa ya shinyanga inavyofanya vizuri katika swala la usafi wa mazingira.” Amesema Mhe. Macha
Katika hatua nyingine Mhe. Macha ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuwaandikisha wanafunzi waliofika umri wa kuanza darasa la awali na darasa la kwanza sambamba na kutowaficha Watoto wenye ulewavu ili wapate elimu bora.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga