- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
RC MNDEME ASISITIZA MUUNGANO ULINDWE KWA NGUVU ZOTE
Na Shinyanga MC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme amesisitiza juu umuhimu wa kuulinda Munngano wa Tanganyika na Zanzibar amabo kesho tarehe 26 Aprili, 2023 ndiuo kilele cha sherehe ambapo sasa unatimiza miaka 59 tangu kuungano kwake.
Msisitizo huo ameutoa leo tarehe 25 Aprili, 2023 katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya wasichana Butengwa ambapo Mkoa umeshiriki katika zoezi la kupanda miti pamoja na kufanya usafinkwenye eneo la shule hiuo iliyopo Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga tukio ambalo liliongozwa naye Mhe. Mndeme akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali, Kamati za Usalama Mkoa na Wilaya, wtumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakoonhozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo, Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa, wakuu wa Taasisi mbalimbali, wadau, wananchi pamoja na wanafunzi.
Rai yangu kwenu nyote, tuhakikishe kwamba Muungano wetu huu tulionao tunaulinda kwa nguvu zetu zote kwakuwa kila mnachokiona hivi sasa kiliasisiwa na viongozi wetu miaka 59 ikiyopita na ndiyo maana mnaona kuna amani, upendo, mshikamano, maendeleo na udugu wetu huu ambao ndiyo imekuwa misingi mikubwa ya Muungano mpaka leo tumekutana hapa tukiwa na amani na vyote hivyo vikiwa vipo, hivyo nasisitiza tena Muungano huu ulindwe kwa nguvu zote tusikubali kabisa kumuona yoyote anauchezea Muungano huu"', alisisitiza Mhe. Mndeme.
Mhe. Mndeme pia amezitaka Halmashauri zote katika Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa unatekelwza maelekezo ya kupanda miti 1500 kwa Halmashauri ipandwe na ifuatiliwe kwa maana ya kutunzwa ili ikue na ije kuwa na tija kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Aidha alitumia muda huo pia kuzitaka Halmashauri kuhakikisha kuwa hazitoi Leseni za Biashara kwa yeyote anayeomba mpaka apewe sharti la kwenda kupanda miti miwili, mmoja wa matunda na mti mwingine wa kivuli, akiisha maliza amuite Afisa Biashara aende akajiridhishe kama kweli ametekeleza sharti hilo kisha ndiyo aje apewe leseni yake ya biashara huku akiwataka kuacha kutoa vibali vya kukata miti.
@ofisi_ya_makamu_wa_rais
@ortamisemi
@ofisi_ya_rc_shinyanga
@shinyanga_press_club
@shinyanga_tanzania
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga