- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika kuadhimisha sikukuu za mwisho wa mwaka zinazoendelea, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa zawadi ya chakula na vitu mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija kilichopo Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Akikabidhi zawadi hizo leo Disemba 28,2024, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amewasihi wanafunzi hao kusoma kwa juhudi ili kufikia ndoto zao, huku akitumia fursa hiyo kuiasa jamii kuachana na imani potofu.
“Shughuli ya leo ni kufikisha zawadi za mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa watoto hawa wenye mahitaji maalumu hapa Buhangija, ili wafurahie sikukuu za mwisho wa mwaka, nitumie Fursa hii kuwaasa muendelee kusoma kwa bidii ili mtimize ndoto zenu msijione wanyonge, Serikali ipo pamoja nanyi kuhakikisha inawatengenezea mazingira rafiki ili muweze kufikia ndoto zenu”. Amesema Wakili Mtatiro
Awali akibainisha zawadi hizi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. Charles Luchagula, ametaja zawadi hizo ni pamoja na unga wa ngano 50, kilo 50 za unga wa semba , kilo 50 za sukari, na mafuta lita 20, juisi na taulo za kike.
Kwa upande wake mwalimu mkuu shule ya Msingi Jumuishi Buhangija Bi. Fatuma Jilala, ambaye ndiye mlezi mkuu wa kituo hicho,amesema kuna Jumla ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu 146, huku akiupongeza uongozi wa Manispaa ya Shinyanga kwa ushirikiano wanaupata kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili shuleni hapo.
Nao baadhi ya watoto hao wenye mahitaji maalumu,wamemshukuru Rais Samia, kwa kuwapatia zawadi hizo za chakula, kwa ajili ya kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka, huku wakimuahidi kusoma kwa bidi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga