- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 30/07/2021 pikipiki 5 zimekabidhiwa kwa kikundi cha Mnarani-boda kutoka Kata ya Kitangili.
Pikipiki hizi zimegharimu jumla ya Shilingi 12,000,000 ambazo ni sehemu ya 10% ya mapato ya ndani ya Manispaa kwako Mwaka wa fedha 2020/2021.
Fedha hizi zinatolewa kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura 290 na kanuni zake zilizotungwa chini ya Kifungu 37A (4) zinazojulikana kama kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu za Mwaka 2019 pamoja na Marekebisho yake yam waka 2021. Pia kwa mujibu wa Mwongozo wa Usimamizi wa fedha na uendeshaji wa akaunti ya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kwa Halmashauri wa mwaka 2020, kifungu 2 (2.6.3).
Jumla ya fedha zitokanazo na 10% za mapato ya ndani zilizotolewa katika mwaka wa Fedha 2020/2021 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenywe Ulemavu ni Shilingi 278,348,419 kwenye vikundi 22 kwa mchanganuo ufuatao: -
Hii inafanya jumla ya Shilingi 1,061,091,419 zilitolewa kwa vikundi 138 vya Wawnawake, Vijana na watu wenye Ulemavu tangu mwaka wa fedha 2015-2016 hadi Juni 30, 2021.
Kikundi hiki cha Boda-Mnarani, kimesaini makataba wa ukopeshaji wa fedha kwa vikundi na kitawajibika kufanya marejesho kuanzia tarehe 01/11/2021 kwa miezi 12 tu. Ikumbukwe kuwa kushindwa kufanya marejesho kwa wakati sheria itachukua mkondo wake, ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa pikipiki hizo na kupatiwa kikundi kingine. Aidha pikipiki hizi zitakuwa chini ya vijana hawa watakaokabidhiwa hapa leo chini ya kikundi chao na sio wengine.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA MAKABIDHIANO
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga