- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
OR- TAMISEMI YATOA MAFUNZO KWA MAAFISA TARAFA NA WATENDAJI WA KATA MANISPAA YA SHINYANGA.
Na . Shinyanga Mc
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( OR- TAMISEMI) leo tarehe 29 Novemba,2023 imeanza kutoa mafunzo kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata yenye lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi
Katika chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM).
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo haya Mwl. Dafroza Ndalichako ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambaye alimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo amewaambia washiriki wawe wasikivu katika mafunzo haya ili wanaporudi katika majukumu yao wawezi kutekeleza kwa waledi.
“Tuwewasikivu katika mafunzo kwani mafunzo haya yatakwenda kuwajengea uwezo wa kufanya majukumu yenu kwa weledi pamoja na kutatua changamoto mbalimbali katika maeneo yenu ya kiutawala ” amesema Mwl. Ndalichako
Mwl. Ndalichako amewasihi Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kwenda kusikiliza na kutatua kero za wananchi, kusimamia miradi ya maendeleo, kusimamia vyanzo vya mapato pamoja na kutoa taarifa kwa wananchi pale fedha za miradi ya maendeleo zinapowasilishwa katika maeneo yao.
Kwa upande wake Ndg. Hamis Mkunga mratibu wa mafunzo kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI amewaeleza washiriki kuwa lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo katika nyanja za utawala, usimamizi wa miradi pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mafunzo haya ya Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata ambayo yatahusisha mada mbalimbali ikiwemo uongozi na Utawala, Maadili ya Utumishi wa Umma, pamoja na Majukumu ya Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata ambapo yatafanyika siku mbili leo tarehe 29 na 30 Novemba, 2023.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga