- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imepokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabara, Wodi na OPD (Jengo la Kitengo cha Wagonjwa wa nje) katika Hospitali ya Kambarage iliyopo mjini Shinyanga.
Katika uzinduzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa Manispaa, Dkt. Jomaary Satura, amesema uboreshaji wa miundombinu unaofanywa katika vituo vya afya umedhamiria kukuza ustawi wa wananchi.
"Tunaendelea kuboresha huduma katika hospitali ili kuwasaidia wagonjwa mbalimbali wanaofika hapa Kambarage.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura akitoa maelekezo kwa wadau wakiwemo Wahandisi waliofika eneo la mradi.
"Lengo letu kubwa ni kukuza na kuboresha ustawi wa wananchi katika Manispaa ya Shinyanga ili wapate huduma bora", amesema.
Baadhi ya wanawake waliojitokeza kwenye uzinduzi wa mradi huo wakishiriki zoezi la kuchimba msingi.
Aidha, Dkt. Satura ameeleza mpaka kufikia mwezi Oktoba mwaka huu, Zahati tano zitakuwa zimeshakamilika kutokana na jitihada wanazozifanya..
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga