- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze amewataka watendaji wa mitaa, vijiji na kata kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wanatoa elimu kwa wananchi juu ya kushiriki kikamilifu katika kupiga kura, kusimamia ukusanyaji wa mapato, pamoja na kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya ndani halmashauri.
Mwl. Kagunze ametoa wito huu leo, Septemba 10, 2025, wakati wa kikao kazi na watendaji wa kata zote 17, mitaa na vijiji, ambapo amesisitiza umuhimu wa mshikamano na ushirikiano wa karibu baina yao, wananchi na viongozi wengine katika kutekeleza majukumu ya kila siku kwa mujibu wa sheria, taratibu na miongozo ya kiutumishi.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Peres Kamugisha, amewataka watendaji kuendeleza juhudi za kudhibiti watoto wa mitaani na kuwawajibisha wazazi wao ili kulinda haki na ustawi wa watoto.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Manispaa manispaa ya Shinyanga, Ndg. Revocatus Lutunda, amewahimiza watendaji kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu zoezi la chanjo za ruzuku linaloendelea kutolewa katika maeneo yao, ili kuhakikisha mifugo inalindwa dhidi ya magonjwa nyemelezi na kuongeza tija katika uzalishaji.
Nao baadhi ya watendaji wa mitaa, vijiji na kata wamemshukuru Mkurugenzi kwa namna ambavyo amekuwa akiendelea kuwakumbusha na kufuatiliaji wa karibu utendaji kazi wao, huku wakiahidi kuendeleza mshikamano na ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao kwa ustawi wa manispaa na wananchi kwa ujumla.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga