- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MWL KAGUNZE AONESHA KUTORIDHISHWA NA KASI YA UJENZI SHULE YA SEKONDARI OLD SHINYANGA
Na. SHINYANGA MC
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze leo tarehe 20 Julai,2023 amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo hususani elimu akiwa ameongozana na wataalam kutoka Manispaa.
Kutokuridhishwa kwa Mwl Kagunze kumetokea wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi na upanuzi wa miundombinu kwa kidato cha 5 unaoendelea katika shule ya Sekondari Old Shinyanga ambapo wanajenga Madarasa [11] Mabweni [4] na Matundu ya vyoo [16] ujenzi huo ambao unaonekana unakwenda kwa kasi ndogo jambo ambalo Mwl. Kagunze kutoridhishwa huku akiwataka mafundi kuongeza kasi kwa kuwa kilakiu kipo.
‘’Sijaridhishwa na kasi ya Ujenzi unaoendelea kwa kuwa kilakitu kipo sioni sababu ya kucheleweshwa ukamiishaji, niwatake muongeze kasi na muda wa ziada wa kufanya kazi ili ujenzi uweze kukamilika kwa haraka’’ alisema Mwl. Kagunze
Sanjali na hilo, Mwl. Kagunze amezitaka kamati za shule kuendelea kutunza nyaraka za ujenzi vizuri,kufuata sheria,miongozo na taratibu za manunuzi bila kukosea Pamoja na kununua samani zenye kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa.
Kipekee Shukrani nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha na kuboresha sekta mbalimbali hususani elimu kwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga