- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MWL. KAGUNZE AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze leo tarehe 12/12/2023 amekutana na wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mwl. Kagunze amekutana na wafanyabiashara hawa kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali pamoja na kuwakumbusha sheria, Kanuni na taratibu za kufuata katika kuendesha biashara za nyumba za kulala wageni.
" tumeitana hapa kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua kero mbalimbali pamoja na kukumbushana sheria, kanunia na taratibu za kufuata katika kuendesha biashara za nyumba za kulala ." amesema Mwl. Kagunze
Akizungumza katika kikao hicho Mwl. Kagunze aliwakaribisha wafanyabiashara waweze kutoa changamoto zao, ambapo waliwasilisha changamoto zikiwemo, kuomba uongozi wa Manispaa kuacha kukagua katika nyumba za kulala muda wa usiku, vitabu vya kuandikia wageni vitolewe bure.
Akijibu changamoto hizi Bi. Naely Somi Kaimu Mkuu Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ameeleza kwamba kutoa vitabu vya wageni bila gharama ni kitu ambacho hakiwezekani kwani wanapotoa fedha za kuchukua vitabu hivyo wanakuwa wamerudisha gharama za utengenezaji pamoja na swala la kuomba uongozi wasikague nyumba za kulala muda wa usiku nalo alijibu ni sheria na taratibu za kufanya ukaguzi muda wa usiku ili kujua wageni wote wanaoingia wanaandika majina katika vitabu vya wageni kwa lengo la usalama.
Pamoja na mambo mengine, wafanyabiashara walipata elimu ya jinsi ya kupambana na majanga ya moto kutoka katika Jeshi la zimamoto na uokoaji, elimu ya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya biashara ili kuepuka magonjwa ya mlipuko, pamoja na kuhamasishwa kuendelea kulipa fedha za uzoaji wa taka ngumu katika maeneo yao.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga