- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MWL.KAGUNZE AKAGUA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI NGOKOLO B
Na.Shinyanga Mc
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze leo tarehe 2 Oktoba, 2023 amekagua Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Ngokolo B inayojengwa katika Kata ya Ndembezi Mtaa wa Butengwa.
Mwl. kagunze amekagua ujenzi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba na kuridhishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea na kuwataka mafundi wasipunguze kasi ya ujenzi na kuwataka wajenge kwa kuzingatia viwango vya kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.
"Nimefurahishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea niwaombe msipunguze kasi ili ifikapo mwezi Desemba, 2023 ujenzi umekamiliki ili mwakani tuweze kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza" alisema Mwl. Kagunze
Shule Mpya ya Ngokolo B Sekondari, Manispaa ya Shinyanga ilipokea kiasi cha Tsh Milioni 603,890,200/= kutoka Serikali kuu ambapo itatumika kujenga Madarasa 8, Jengo la Utawala 1, Matundu ya Vyoo 22, Jengo la Tehama 1,Maktaba 1 na Maabara 3.
Kukamilika kwa ujenzi huu wa Shule utasaidia kupunguza Msongamano kwa wanafunzi wanaojazana kwa wingi katika shule ya Sekondari Ngokolo ambapo wengi huchaguliwa katika shule hiyo.
Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezesha Sekta zote hususani Sekta ya elimu Manispaa ya Shinyanga.MWL.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga