- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MWL. KAGUNZE AFANYA KIKAO KAZI NA WATENDAJI WA KATA , VIJIJI NA MITAA MANISPAA YA SHINYANGA.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze leo tarehe 20 Oktoba, 2023 amefanya kikao kazi na Watendaji wa Kata, Mitaa pamoja na Vijiji katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna ulipo katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza katika kikao Mwl. Kagunze amewapongeza watendaji kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo pamoja na kusimamia vizuri majukumu ya kila siku katika sehemu zao za kazi.
"Niwapongeze kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika maeneo yenu ya kazi pamoja na usimamizi mzuri katika kuhudumia wananchi " alisema Mwl. Kagunze
Aidha, Mwl. Kagunze amewaagiza watendaji kwenda kusimamia kwa ukaribu mambo mbalimbali yakiwemo kutenga siku moja ya wiki ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi, kufanya mikutano ya hadhara kila mwezi kwa kuwasomea mapato na matumizi katika maeneo yao ya kiutawala pamoja na kutoa taarifa ya utekelezaji wa vikao na mikutano iliyofanyika kila mwezi.
Pia amewataka kwenda kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti na kulinda miti iliyokwisha pandwa, kusimamia mapato ya ndani, kudhibiti utoro kwa wanafunzi, kusimamia ulaji wa chakula mashuleni, kusimami miradi ya maendeleo, kutoa taarifa za fedha zinapoingia kwenye akaunti za kata kwa ajili ya miradi kwa wananchi pamoja na kuendelea kutoa taadhari ya mvua ya El Nino kwa wananchi.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Ndg. Said Kitinga pia amewataka watendaji kufahamu na kufuatilia kila miradi inayoendelea kutekelezwa katika kata zao pamoja na utoaji wa taarifa uzingatie ngazi za kiutawala.
Pamoja na mambo mengi Mwl. Kagunze alipata wasaa wa kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za watendaji ambazo waliziwasilisha na nyengine alizichukua kwa ajili ya kuzifanyia kazi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga