- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MWL. KAGUNZE AAGIZA WAZAZI WARUDISHIWE FEDHA ZA MICHANGO WALIZOCHANGA KIMAKOSA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze ameagiza shilingi 4,475,000/= zilizolipwa kimakosa na wazazi wa wanafunzi waliojiunga kidato cha kwanza Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga (Shinyanga Girls Secondary School) iliyopo kata ya Ndembezi zirudishwe kwa wazazi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Januari 20, 2024 Mwl. Kagunze amesema maagizo hayo ameyatoa kwa uongozi wa shule na maafisa elimu wilaya na kata kwamba wasimamie kuhakikisha fedha zote zinarejeshwa kwa wazazi.
“Nimeagiza wazazi wote ambao kimakosa walijikuta wamechukua fomu ya kujiunga kidato cha tano kwa shule za bweni badala ya fomu ya kujiunga kidato cha kwanza warejeshewe fedha zao shilingi 80,000/= (mchanganuo ni shilingi 65,000/= kwa ajii ya uendeshaji wa shule, Tahadhari 5,000, nembo ya shule 5,000/= na kitambulisho cha shule 5, 000/= tayari fedha zao jumla shilingi 4,475,000/= zimetolewa kwenye akaunti ya shule na tayari wazazi wameanza kurudishiwa fedha zao”. amesema Mwl. Kagunze.
Aidha, Mwl. Kagunze amewata maafisa elimu wilaya na kata wasimamie kuhakikisha kwamba fedha zote zirejeshwe kwa wazazi na risiti zote azione na kama ni SMS za miamala ya simu azione ili kumaliza mkanganyiko huo uliotokea, ambapo baadhi ya wazazi wamekiri kupokea fedha walizochanga kwa wale waliopo ndani ya mkoa wa Shinyanga wamefika shuleni wakachukua na wameshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu kwa kuwajengea hii shule kwa gharama ya shilingi Bilioni 4.1 na elimu ni bure kwa wanafunzi wote.
Pamoja na mambo mengine Mwl. kagunze amewakaribisha wanafunzi wote wa kidato cha kwanza,ambapo mpaka kufikia leo jumla ya wanafunzi 100 wameripoti shuleni kati ya 143 ambao wamepangiwa kujiunga kitado cha kwanza katika shule ya sekondari ya wasichana.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga