- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MWENYEKITI WA WAZAZI CCM TAIFA ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI BUTENGWA MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Mwenyekiti wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Fadhil Maganya leo tarehe 9 March, 2024 amefanya ziara ya kukagua na kutembelea Shule ya Sekondari Butengwa iliyopo katika kata ya Ndembeze Manispaa ya Shinyanga.
Ndg. Maganya ametembelea na kukagua Shule mpya ya Sekondari ya Butengwa na kuonesha kuridhishwa na ujenzi wa shule hiyo na kuwasihi walimu kuendelea kuwasimami wanafunzi waendelee kuwa nadhifu na wenye maadili mema.
“Niwapongeze kwa ujenzi mzuri hakika mmeitendea haki pesa iliyotolewa na Serikali Binafsi nimeridhishwa na ujenzi na niwaombe muendelee kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi inayoletwa kwa kuzingatia thamani ya pesa , lakini pia tuendelee kuwahimiza wanafunzi wetu waendelee kuwa nadhifu na wenye maadili mema kwani elimu bora inaambatana na maadili mema”. amesema Ndg. Maganya
Pamoja na mambo mengine Ndg. Maganya alipata wasaa wa kuongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Butengwa na kuwasihi wasome kwa bidii ili wawezi kufikia ndoto zao kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amekwisha waandalia mazingira bora ya kupata elimu iliyobora huku akiwasifia kwa unadhifu wao na kuwaomba kuendelea kuwa nadhifu kila siku.
Shule ya Butengwa ilitumiwa kiasi cha milioni 603,890,562 kutoka serikali kupitia Mpango wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa ajili ya kujenga Madarasa 8, jengo la utawala, Maktaba, jengo la Tehama, Matundu ya vyoo 8, maabara ya fizikia, maabara ya kemia na Bailojia , tanki la maji ardhini pamoja na kichomea taka ambapo mpaka sasa majengo hayo yameweza kujengwa.
Aidha, Shule ya Sekondari Butegwa ni Shule mpya ambayo imeanza mwaka huu kwa kupokea kidato cha kwanza 2024 na kupitia ujenzi wa Shule hii imesaidia kupunguza idadi kubwa ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Ngokolo na Mazinge zilizokuwa na idadi kubwa ya Wanafunzi shukrani kwa Rais wetu kwa kuendelea kuwezesha sekta zote Manispaa ya shinyanga hususani sekta ya elimu.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga