- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Zoezi la kuwasajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa bila malipo watoto wote walio na umri chini ya miaka 5 linaendelea katika kila ofisi za mtendaji wa kata na vituo vya afya vinavyotoa huduma ya mama na mtoto. Katika picha Bi.Evelyne Afisa Muuguzi Msaidizi katika kituo cha Afya cha Magereza, kilichopo mtaa wa Ushirika, kata ya Chamaguha, Manispaa ya Shinyanga akimkabidhi Bi. Esther Elias (Mzazi wa Loveness Juma Charles) cheti cha kuzaliwa baada ya kusajili katika daftari la usajili. Unaweza kuona mahojiano kati ya Afisa Muuguzi Msaidizi na Bi.Esther Elias wakati wa usajili wa mtoto kwa kubonyeza hapa.
Mara baada ya kusajili na kupokea cheti cha kuzaliwa wazazi huelemishwa kuwa cheti kinachotolewa ni halali kwa matumizi yoyote. Na pia cheti hakina ukomo wa matumizi ya mtoto hatalazimika kupata cheti kingine baada ya umri wa miaka 5. Kwa hiyo ni vema cheti kitunzwe mahali salama na kisikunjwe.
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa usajili na utoaji wav yeti vya kuzaliwa ni kama ifuatavyo:
Umuhimu wa Cheti cha Kuzaliwa
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Manispaa anaendelea kutoa wito kwa wananchi wote kuwaleta watoto wote walio na umri chini ya miaka 5 ili wasajiliwe na kupewa vyeti vya kuzaliwa. Baada ya muda serikali itaanza zoezi la ukaguzi wa kubaini watoto wote chini ya umri wa miaka 5 ambao hawana vyeti vya kuzaliwa na kuchukua hatua stakihi dhidi ya wananchi waliokaidi kuwapatia haki ya kupata cheti cha kuzaliwa.
“Mtoto anastahili cheti cha kuzaliwa, Mpe haki yake”
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga