- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko, amewataka wananchi walio ndani ya Manispaa kuhakikisha wanaiunga mkono Serikali katika zoezi ulipaji wa tozo mbalimbambali ambazo zinatozwa na Halmashauri ili kukuza ustawi wa maendeleo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias R. Masumbuko akizungumza na Wananchi wa Ngokolo.
Hayo ameyasema leo Machi 31, 2023 wakati wa Ufunguzi wa Choo cha Kisasa kilichojengwa katika Soko la Ngokolo Mtumbani kwa gharama ya Fedha za Mapato ya ndani kutoka Halmashauri.
Mhe. Masumbuko amesema Manispaa ya Shinyanga imekuwa ikijipanga kila siku kuboresha miundombinu kwa wananchi ili kuboresha huduma ikiwemo ukusanyaji wa tozo.
“Sisi kama Manispaa tunaendelea kujipanga ili kuboresha huduma kwa wananchi, fedha zinazotumika kujenga miundombinu ndizo hizi zinazochangia kujenga na kuboresha miundombinu ambayo mnaiona hivi sasa ikiwemo ujenzi wa hiki Choo cha Kisasa.
“Kile ambacho tumekikusanya kwenu tunazidi kuomba ushirikiano wa kutosha ikiwemo kutuunga mkono katika tozo mbalimbali ambazo mnapaswa kutoa, ili kuisaidia Serikali kukuza ustawi wa maendeleo katika jamii. amesema Mh. Masumbuko.
Aidha, Mstahiki Meya ameongeza kwa kuwataka wananchi wakitunze Choo hicho kilichojengwa kwa miundombinu ya kisasa ili kiweze kudumu kwa muda mrefu, sambamba na kuzingatia usafi katika matumizi.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Ngokolo, Mhe. Victor Mkwizu, amesema Miradi yote inayoendelea ndani ya Manispaa ikwemo ujenzi wa Choo cha Kisasa Ngokolo inatokana na Utekelezaji Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mhe, Mkwizu ameeleza kikao alichowahi kuitisha na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Jomaary M. Satura juu ya ujenzi wa Choo cha Kisasa Ngokolo, kimeleta matokeo chanya na akiwaomba wananchi kukitumia vizuri.
Diwani wa Kata ya Ngokolo, Mhe. Victor Mkwizu akizungumza katika halfa ya ufunguzi wa Choo cha Kisasa Ngokolo Mtumbani.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John R. Tesha, amesema lengo la Manispaa kuendea kuboresha miundombinu ni kuboresha mazingira kwa wananchi ikiwemo ujenzi wa vyoo vya kisasa ambavyo vitajengwa katika masoko yote.
Mbali na ujenziwa Choo cha Kisasa Ngokolo, Tesha ameainisha kuwa Manispaa itaendelea kujenga miradi mbalimbali mingi ya maendeleo ikiwemo Stendi za Daladala, Masoko ili kuboresha mazingira ya huduma nzuri kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, John R. Tesha akizungumza katika halfa ya ufunguzi wa Choo cha Kisasa Ngokolo Mtumbani.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga