- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Elias R. Masumbuko amewataka wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuchukua hatua za dharura kutengeneza barabara inayoelekea katika dampo kuu la ukusanyaji taka lililoko katika kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki meya ametoa agizo hili leo Novemba 01, 2024 katika mkutano maalumu wa baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga lilikoketi leo kwa siku ya pili katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ikiwa ni mkutano wa kwanza wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 wenye lengo la kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Pamoja na uwasilishaji wa taarifa za utendaji kazi kwa taasisi mbalimbali za umma ndani ya Manispaa.
“Kazi kubwa inayofanywa na uongozi wa manispaa ya Shinyang Chini ya mkurugenzi wetu ni Kuhakikisha manispaa hii inakuwa na mazingira safi, ndiyo maana hata tuzo ya usafi tulishinda sisi, agizo langu kwa TARURA nendeni mkahakikishe barabara hiyo mnaikarabati ili magari yanayokusanya taka yaweze kupita kwa urahisi katika msimu huu wa mvua”. Amesema Mhe. Masumbuko
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewasihi wadiwani kuendelea Kuwapa elimu wananchi juu ya umuhimu kwa wananchi kujitokeza kupiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu ikiwa ni haki yao ya kikatiba.
“Ndugu zangu Waheshimiwa Madiwani sote tunatambua Novemba 27 mwaka huu tunauchaguzi wa viongozi wa Mitaa na Vijiji,tuendelee kuwapa elimu wananchi kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi huo, Itakuwa haina maana kama tumejiandikisha harafu tusiende kupiga kura, maendeleo yoyote kwenye kata yanachagiwa na viongozi bora ninawaomba sana twendeni tukawahamasishe wananchi wakapige kura” Amesema RC Macha.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga