- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo tarehe 15/09/2021 amefanya mkutano na wafanyabiashara wa soko la Chamaguha na soko la Machinga. Mkuu wa mkoa aliongozana na Mkuu wa Wilaya, Mkurugerunzi wa Manispaa ya Shinyanga pamoja na Afisa Biashara, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Mipango Miji, Afisa Utumishi na Afisa TEHAMA.
Mkutano ulifunguliwa na Mkuu wa Wilaya na baadaye kuwakaribisha wafanyabiashara kutoa changamoto zinazowakabili.
Mwenyekiti Msaidizi wa soko la chamaguha alitoa mojawapo ya changamoto ni miundombinu ya barabara kuwa mibovu na wakati wa masika kushindwa kutumika hivyo kuomba kuboreshwa kwa wakati.hata hivyo Mwenyekiti huyo alimpongeza Mkurugenzi kwa kujitahidi kutatua changamoto nyingi zilizokuwa zikiwakabili.
Mkurugenzi wa Manispaa ya shinyanga alipata nafasi ya kuzungumza na wafanyabiashara na kuwashukuru kwa kuhama kutoka soko la Kambarage bila shuruti, aliwaambia kuwa lengo kuu la Serikali ni kufanya biashara zao kukua na kuwa chachu ya maendeleo ya Manispaa ya Shinyanga.
Vivyo hivyo Mkurugenzi aliwaahidi kuwapa ushirikiano katika ukuaji wa soko kwa kuboresha miundombinu kama vile kuongeza idadi ya vyoo ili kuweza kutosheleza mahitaji ya wafanyabiashara pamoja na wateja kwa idadi.
Aidha katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa alizungumza na wafanyabiashara na kuwashukuru kwa kukubali kuhama kutoka soko la Kambarage na kuhamia soko jipya la Chamaguha kwa kufuata ushauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwenye matumizi ya sera ya Diplomasia na Maelewano.
Mkuu wa Mkoa amemshukuru Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga na viongozi wengine kwa kuweka mazingira sawa mpaka soko kuanzishwa.
Pia Mkuu wa Mkoa amesema kwa kushirikiana na Manispaa ya Shinyanga amewaahidi wafanyabiashara hao kuendelea kuwaboreshea miundombinu ya soko hasa kwa kuanza na urekebishaji wa barabara ili kuwe na mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao.
Pia Mkuu wa Mkoa aliwahakikishia wafanyabiashara wote katika soko la mbao la Chamaguha kuwa eneo hilo ndilo litakalokuwa eneo pekee la kuuza mbao pamoja na bidhaa za mazao ya misitu.
Akiwa katika soko la Machinga lililopo kata ya mjini, Mkuu wa Mkoa alikutana na wafanyabiashara ambao pia alisikiliza kero zao ikiwa ni Pamoja na ukosefu wa maji, miundombinu mibovu ya barabara, vibanda vya wafanyabiashara kutokuwa na ubora na kuhofia changamoto kubwa wakati wa masika, pia waliomba kuwepo na mnada siku ya jumatano ya kila wiki.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa aliwapa moyo wafanyabiashara hao kwa kuahidi kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kutatua changamoto zao zote. Aliwaahidi kulitangaza soko hilo kuwa rasmi na kulifanyia ufunguzi.
Viongozi wa soko la Machinga waliwasisitiza wafanyabiashara wenzao kutimiza majukumu yao kwa kulipia vitambulisho vya wajasiriamali wadogo ili kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa na bugudha ama usumbufu.
MATUKIO KATIKA PICHA
Soko la mbao Chamaguha
Mkuu wa Mkoa akisikiliza Wafanyabiashara
Wafanyabiashara wakisikiliza kwa makini
Mkuu wa Mkoa akitembelea soko la mbao
Soko la Machinga
Mkuu wa Mkoa akisikiliza changamoto za
Wafanyabiashara wa soko la Machinga
Mkuu wa mkoa akitembelea Soko la Machinga
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga