- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze amewataka walimu kuzingatia maadili yao ya kazi ili kuleta tija kwenye sekta ya elimu.
Mwl. Kagunze ameyasema hayo leo tarehe 6 Agosti, kwenye kikao kazi cha walimu wa sekondari, waratibu elimu sekondari,maafisa elimu kata Pamoja na wathibiti ubora elimu ngazi ya sekondari wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Buhangija chenye lengo la kujadili na kusikiliza maelekezo na utaratibu wa utumishi sekta ya Elimu na kuwataka walimu kutimiza wajibu wao.
“Kila Mwalimu atende wajibu wake kwa kuzingatia haki,kila mwalimu apewe haki yake tusinyanyasane mwalimu mkuu akikuagiza kazi timiza nia yetu ni kufanya Manispaa ya Shinyanga ifanye vizuri katika mitihani ya taifa”. amesema Mwl. Kagunze.
Katika hatua nyingine Mwl. Kagunze amekemea tabia ya walimu wakuu wa shule za sekondari wanaotumia madaraka yao vibaya kwa ajili ya kuwakandamiza walimu wengine.
Kwa upande wake Afisa Elimu sekondari Manispaa ya Shinyanga Mwl. Lucas Mzungu ameahidi kuwasimamia na kuwakumbusha miiko ya kazi pamoja na kuhakikisha kila mwalimu anapata haki yake pasipo kukiuka taratibu za kazi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga