- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wakandarasi na Mafundi (local fundi) wate wanaotumia vibaya rasilimali na vifaa vya kujengea katika miradi yote inayotekelezwa ndani ya manispaa huku akiwataka kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Mwl. Kagunze ametoa maagizo hayo leo Disemba 17,kwenye mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwataka wakandarasi pamoja na mafundi ( Local Fundi) kulipa fidia za rasilimali za serikali pale wanapotumia kinyume na utaratibu.
“Mnachanyanga saruji pamoja na mchanga harafu hamtumii kwa wakati huo, matokeo yake mnaharibu hali ambayo mnaipelekea serikali hasara, sitamfumbia macho mkandarasi au fundi yoyote anayetumia hovyo rasilimali au vifaa vya ujenzi wa miradi ya serikali, Serikali inatoa fedha nyingi kujenga na kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi ,hivyo nakuagiza Mhandisi wa halmashauri kuwachukulia hatua wakandarasi pamoja na mafundi kulipa fidia na kuwaandikia barua ya onyo ili tabia hizi zisijirudie katika manispaa yetu”. Amesema Mwl. Kagunze.
Katika hatua nyingine Mwl. Kagunze amempongeza Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Ihapa Dkt. Consolath Mpepera kwa hatua alizichukua za kuanza kupanda miti katika kituo hicho huku akimwagiza kuendelea kupanda miti elfu moja na kuitunza katika eneo lote linalozunguka kituo hicho.
Mwl. Kagunze amefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya afya na elimu ambapo katembelea ujenzi wa nyumba ya walimu Butengwa Sekondari, Ujenzi wa mabweni manne shule ya sekondari Rajani kata ya Ibadakuli, Ujenzi wa vyumba vitatu shule ya msingi Ndala “B’’, ujenzi wa vyumba vitatu na vyoo shule ya msingi Nheregani, Ujenzi madarasa matatu, matundu ya vyoo matano na chumba kimoja cha kujistiri wanafunzi wa kike shule ya msingi twendepamoja pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Ihapa kata ya Old Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga