- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze ameagiza kun’yang’anywa majengo mawili kati ya nane aliyopewa Mkandarasi wa Kampuni ya CBAM Global Co.Ltd ambayo utekelezaji wake umeshindwa kwenda na kasi kadri ya mkataba wake.
Mwl. Kagunze ametoa maagizo haya leo Disemba 16,2024 alipofanya ziara ya kushtukiza na kukagua ujenzi wa shule hiyo mpya ya sekodari inayojengwa katika kata ya Kizumbi.
“Mkandarasi huyu ana jumla ya majengo nane katika mradi huu wa shule, lakini utekelezaji wake uko chini sana, hivyo naelekeza anyang’anywe majengo yote yaliyopo katika hatua ya msingi ,ili apatiwe mkandarasi mwingine mwenye uwezo wa kumaliza ndani ya wakati “. Amesema Mwl. Kagunze”
Aidha Mwl. Kagunze amechukua hatua hiyo, ikiwa ni siku kumi na moja tangu alipofanya ziara ya kushtukiza Disemba 5,2024 ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo inayojengwa katika kata ya Kizumbi ikilenga kupunguza muda wa wanafunzi wanaosafiri umbali mrefu kutoka nyumbani.
Katika hatua nyingine Mwl. Kagunze ametumia nafasi hii kumpongeza fundi asiye Mkandarasi (Local Fundi) anayetekeleza ujenzi wa jengo la utawala katika shule hiyo, kwa kazi nzuri na yenye ufanisi inayoendana na kasi hitajika.
Majengo ambayo ameagiza kunyang’anywa mkandarasi huyo ni pamoja na jengo la Maabara ya Baiolojia, Kemia na Maabara ya Fizikia yaliyokwama yakiwa katika hatua ya ujenzi wa Msingi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga