- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg Jomaary Mrisho Satura leo tarehe 09/09/2021 ametembelea baadhi ya maeneo ya kata ya Ibinzamata, Stendi ya Mkoa na maeneo yanayozunguka Stendi na kujionea Uchafu uliokithiri.
Pia alitembelea eneo la relini lililopo kata ya Chamaguha na kujionea hali mbaya ya uchafu wa Muda mrefu.
Katika msafara huo aliongozana na Mtendaji wa kata ya Ibinzamata, kata ya Chamaguha, Afisa Utumishi, Afisa TEHAMA na Afisa Afya.
Akiwa katika hali ya masikitiko makubwa, Mkurugenzi alitoa maagizo kwa Watendaji wote Pamoja na Afisa Afya kuhakikisha Mji katika maeneo yao unakuwa safi kufikia kesho tarehe 10/09/2021.
“Toka siku ya kwanza naingia katika Manispaa ya Shinyanga niliona uchafu mwingi, nikajipa moyo labda utazolewa lakini hali iko vilevile toka siku ya kwanza, Watendaji mpo lakini hamfanyi kazi yenu ipasavyo. Mimi nafanya kazi na watu wanaojielewa na huwa sina ushikaji kwenye kazi”. Alisema Mkurugenzi. “Naagiza uchafu wote uzolewe na kusiwepo na aina yoyote ya takataka kufikia kesho.” Aliongeza.
Alitoa mfano wa Mkoa wa Njombe jinsi ulivyo safi na Madereva wakashuhudia jinsi barabara za Mkoa wa Njombe zilivyo bora na safi kiasi kwamba unawezafikiri zinasafishwa kwa maji.
Mkurugenzi amewataka Watumishi kubadilika na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika maeneo yao.
MATUKIO KATIKA PICHA
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga