- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tarehe 3/09/2021 Mkurugenzi wa Manispaa Ndg Jomaary Mrisho Satura alikutana na Wafanyabiashara mbalimbali kufanya majadiliano kwa maslahi pana ya Maendeleo ya Manispaa ya Shinyanga.
Kikao hicho kilifanyika mnamo saa 11 jioni katika Hotel ya Empire, lengo kuu ni kuwa na Muono wa Pamoja juu ya masuala mbalimbali ya Biashara na Maendeleo.
Katika kikao kazi hicho Mkurugenzi aliambatana na Wataalamu(Wakuu wa Idara na Vitengo) kutoka Ofisi za Halmashauri ya Manispaa kama ifuatavyo, Afisa Utumishi, Afisa Mipango, Afisa Biashara, Mweka Hazina, Afisa Maendeleo ya Jamii na Afisa Tehama
Pia Madiwani ambao ni wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala walishiriki.
Mkurugenzi aliwahakikishia Wafanyabiashara Kutatua Changamoto zao zinazowakabili kwa Maendeleo ya Manispaa ya Shinyanga, “Kukiwa na Tatizo ama Changamoto yoyote tuiteni,nipo tayari mimi na Wataalamu wangu, Tutakuja”. Alisema Mkurugenzi.
Mkurugenzi alielezea kwa kirefu jinsi ambavyo ni muhimu sana kujenga Mahusiano bora kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo/Wafanyabiashara.
Aidha Mkurugenzi ameelezea changamoto mbalimbali zinazokwamisha Maendeleo ndani ya Manispaa ya Shinyanga ikiwemo Idadi ndogo ya watu, Pamoja na watu wengi kutegemea kilimo. “Changamoto kubwa ndani ya Manispaa yetu ni uwepo mdogo wa watu wanaoishi, kuingia na kutoka.Jambo hili linaathiri sana ukuaji wa Uchumi”. Alisema Mkurugenzi kisha akaongeza, “60% ya wakazi wa Shinyanga ni wakulima, wanalima eneo dogo lililopo, hali inayoathiri uwekezaji na ukuaji wa Uchumi”.
Mkurugenzi alisema Halmashauri inakusudia kuendeleza kilimo cha kisasa katika maeneo ya Tangayika Parkers na Chibe kwa lengo la kukuza Viwanda na uwekezaji wa Kilimo katika Maeneo madogo tuliyonayo.
Akiendelea kuwakumbusha umuhimu wao wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa Maendeleo alisema Serikali haifanyi Biashara bali hujiendesha kwa Tozo na Kodi mbalimbali.
Baada ya Maelekezo mazuri na ya kina kutoka kwa Mkurugezi, Majadiliano yalifunguliwa rasmi na wafanyabiashara wakatoa maoni yao..
Mwenyekiti wa Soko la Nguzonane aliomba Halmashauri iwashirikishe Wafanyabiashara kabla ya kutekeleza shughuli zake, mfano kabla ya kuendesha Oparesheni za Mapato Halmashauri iwashirikishe viongozi wa Masoko ambao nao watazungumza na wafanyabiashara ili kuwapatia uelewa wa Pamoja juu ya tozo na kodi za Serikali. Pia akasistiza kutolewe risiti kila mara Halmashauri inapodai Kodi la sivyo itaonekana kodi hiyo ni batili.
Majadiliano yaliendelea katika hali ya uelewano mkubwa huku kila upande ukiwa na shauku ya kuiendeleza Manispaa, mjumbe mwingine Dr. Haraka ambae ni mmiliki wa Hotel ya Empire alitoa mchango wake kwa kusema ili idadi ya watu iongezeke Halmashauri iandae utaratibu wa kujenga vyuo vikuu na vyuo vingine vidogo. Pia aliomba barabara zijengwe kwenda maeneo ya kimkakati ya kibiashara kama vile Kambarage HC, Karena Hotel n.k. Kwa Kumalizia aliiomba serikali kuangalia upya tozo mbalimbali hususani katika Hotel.
Mama Karena ambaye ni mmiliki wa Hotel,alisema Halmashauri iache kulimbikiza kodi za Hotel kwani inaathiri kiwango cha ulipaji wa kodi hizo. Pia aliiomba Halmashauri iboreshe utaratibu wa kukagua Mahotel bila kutumia vitisho ama silaha.
Mjumbe mwingine aliyechangia ni Kiongozi wa Machinga ambae aliomba Masoko ya Machinga yawekewe miundombinu mizuri ya kuvutia ukuaji wa biashara pia elimu itolewe kwa wafanyabiashara kujenga uelewa zaidi.
Mwenyekiti wa Mama Lishe alitoa rai kwa halmashauri kuwa idhibiti mama Lishe wanaouza vyakula vyao nje bila ya kuwa na vizimba ndani ya soko jambo linaloathiri kukosekana kwa wateja ndani ya soko kwa Mama Lishe wenye vizimba. Pia aliiomba Halmashauri Kuweka soko kubwa la Mazao la Kimataifa ili kuhudumia Maeneo mbalimbali ndani ya nchi yetu.
Wachangiaji wengine waliomba Maafisa Afya watazamwe upya kwani wamekuwa kero kubwa kwa wafanyabiashara. Pia wamiliki wa Malori watengewe eneo la Malori Kwa ajili ya Malori.
Mkurugenzi wa Manispaa aliahidi kushughulikia kero zote na zile ambazo wao wanadhani ni kero lakini wakati mwingine ni kwa sababu ya uelewa basi wataeleweshwa na elimu mbalimbali zitaendelea kutolewa ili kuwepo na uelewa wa Pamoja na kujenga mahusiano imara.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga