- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Madawati 2500 kwa shule za msingi, viti na meza 2500 kwa shule za sekondari itawezesha wanafunzi wote kuanzia chekechea hadi Sekondari kukaa katika madawati.hii inakwenda sambamba na kumsapoti Rais wetu mama Samia ambae amekuwa na msukumo mkubwa katika utoaji huduma kwa jamii, ambapo sh trillion 1.3 zilizotolewa katika mpango wa covid19 Manispaa imepokea million 880 kwa ajili ya ukamilishaji wa madarasa 35 kwa shule za sekondari na madarasa 9 kwa shule shikizi.Katika kumuunga mkono mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Manispaa ya Shinyanga imetumia mapato yake ya ndani kutengeneza madawati 2500 kwa shule za msingi, viti na meza 2500 kwa shule za sekondari.ambapo Mwenyekiti wa Wafanyabiashara ndg Shuma alialikwa ili ashuhudie kuwa sehemu ya fedha wanayotoa wafanyabiashara kama kodi inatumika kwa ajili ya maendeleo. Utengenezaji wa madawati , viti Pamoja na meza utatoa fursa kwa wanafunzi Zaidi ya 50 wa VETA katika fani ya useremala na uchomeleaji kujifunza kwa vitendo.
Mchakato wa kutengeneza madawati uliwashirikisha wanajamii wote na ulipitia michakato yote ya manunuzi na VETA wakaibuka kidedea kwa kuwa wao ndo walikuwa the lowest bider na pia wana miundo mbinu ya kisasa ya Serikali katika kufanya kazi hiyo.
Mkuu wa Chuo cha VETA ametoa shukrani zake kwa uongozi wa Manispaa kwa kukubali kufanya kazi Pamoja.
Mwenyekiti wa Kamati za Huduma, Uchumi, Elimu na Afya Mheshimiwa Nkwabi alifurahishwa na mkataba huo wa ujenzi wa madawati ambapo alisema ile ndoto ya kuwa wa kwanza kitaifa inaenda kutimia na ndoto ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuwa jiji pia inaenda kufanikiwa.” Mkuu wetu, zile ndoto za Halmashauri ya Shinyanga kuwa jiji zinaenda kutimia, tunapotoa ujinga sasa ni dalili njema kuwa tunaelekea kwenye mafanikio”. Alisema Mheshimiwa Nkwabi.Alimaliza kwa kutoa shukrani zake na kuahidi kuwa kamati itatoa ushirikiano mkubwa kwa Mkurugenzi Pamoja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuhakikisha mikakati yote ya maendeleo inafanikiwa kwa ufanisi mkubwa.
Pia Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Ndg. Shuma Madulu alitoa shukrani zake kwa Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya kwa kuonyesha uwazi katika masuala yote yahusuyo maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. “Nimshukuru Mkurugenzi, kwa sababu Wakurugenzi waliopita Shinyanga ni wengi lakini kwa utandawazi huu amekuja kutuonyesha wafanyabiashara kushuhudia na kutukumbuka kuwa nasi ni wachangiaji wakuu katika maendeleo kitu ambacho hapo nyuma hakikuwahi kufanyika. Naomba Mkurugenzi aendelee Pamoja na Mkuu wetu wa Wilaya ambae amekuwa akisisitiza maendeleo akiamini Maendeleo ndani ya Shinyanga yetu yanawezekana”. Alisema Ndg Shuma.
Aidha kwa nyakati tofauti, Afisa Elimu Msingi na Sekondari Walitoa shukrani zao za dhati hasa wakizingatia kuwa miradi hiyo inawalenga wao moja kwa moja.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mheshimiwa Makune alitoa shukrani zake kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia kwa kuleta fedha kwa ajili ya mipango ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kisha akapata wasaa wa kumkaribisha Mkuu wa Wilaya Bi Jasinta Mboneko ili aseme machache kabla ya tukio la kusaini mkataba kuanza.
Mkuu wa Wilaya alianza kwa kuipongeza Halmashauri kwa hatua nzuri na Madhubuti ya kuhakikisha Miundo mbinu ya darasani inaimarika na kwamba kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati ili kufanya zoezi la kujifunza liwe Rafiki kwa wanafunzi na walimu pia alimpongeza Mkurugenzi Pamoja na Kamati za Huduma, Uchumi, Elimu na Afya kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta Maendeleo. “Tukiacha wanafunzi twende kwa Walimu kwa sababu na wao katika mazingira ya Ufundishaji lazima wakae sehemu nzuri, kwa kuzingatia hilo mimi binafsi kama mkuu wa Wilaya nimekwishaanza kupeleka Meza na viti katika baadhi ya shule”. Alisema Bi. Mboneko. Alisisitiza Walimu kutoa majaribio kila wiki ili kuwaandaa Watoto wasiogope mitihani na kuwafanya wapate ufaulu mzuri.
Baada ya Hotuba fupi ya Mkuu wa Wilaya Mkataba ulisainiwa na pande zote.
Hafla hiyo fupi ya utiaji Saini mkataba huo ilifanyika katika ukumbi wa VETA tarehe 28 Oktoba 2021 Alhamisi huku ikishuhudiwa na Wataalamu kutoka Manispaa, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara, Mkuu wa Wilaya, Mstahiki Naibu Meya, Mwenyekiti wa Kamati za Huduma, Uchumi, Elimu na Afya na baadhi ya Watumishi kutoka VETA.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga