- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na George Mganga, Shinyanga Manispaa
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Mh. Sophia Mjema, amevitaka vikundi vilivyopata mkopo wa Pikipiki kutumia vyombo vya usafiri kwa kuzingatia sheria za usalama bararabani.
Rai hiyo ameitoa leo Disemba 2, 2022, wakati wa ukabidhishaji mikopo kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwenda kwa vikundi tisa (9) yenye thamani ya Tshs. Milioni mia moja arobaini na nne, laki nne na elfu ishirini nan ne (144,424,00).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mh. Sophia Mjema, akizungumza katika hafla ya ukabidhishaji mikopo kwa makundi 9.
Akikabidhi mikopo hiyo iliyotolewa na Manispaa kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa kipindi cha robo ya pili ya 2022/2023, Mjema amesisitiza utii wa sheria bila shuruti, akieleza ndiyo kinga kuu ya usalama barabarani.
“Mmepata pikipiki hizi nzuri, sasa ni wakati wa kwenda kuzitendea haki huko kwa kuzingatia sheria zilizowekwa. Naomba zisiende kutumika katika uhalifu bali kazi iliyokusudiwa.
“Muache kupakiza mizigo ambayo haiendani na pikipiki, tunaona wengine wamekuwa wakipakiza mbao ambazo zinachukua nafasi kubwa ya barabara, hili halitakiwi, kuna magari maalum ya kubeba hizo mbao, na mtakaokiuka maagizo, hatua za kisheria zitachukuliwa”, amesema Mjema.
Kwa upande mwingine, Mh. Mjema amewaasa wanavikundi wote waliopewa mikopo, waende kuitumia kwa makusudio ya miradi pekee na si vitu vingine ili waweze kurejesha, huku akitoa msisitizo wa kufanya marejesho haraka na kwa wakati mwafaka.
Wanakikundi waliopewa mkopo wa Pikipiki katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mh. Jasinta Mboneko.
Wakati huo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mh. Jasinta Mboneko ameeleza kuwa watashiriki kikamilifu kusimamia zoezi la urejeshaji wa mikopo iliyotolewa na Manispaa ili kuwasaidia wengine pia kukopeshwa sambamba na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki.
“Tutaendelea kutoa elimu ya usalama barabarani ili kuepusha ajali ambazo zinapunguza nguvu kazi ya taifa, mbali na hilo pia tutahakikisha mikopo yote iliyokopeshwa inarejeshwa kwa wakati ili kusaidia wengine." amesema Mboneko.
Naye Mh. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Elias Masumbuko, ameongeza kwa kusema kuwa Vijana, Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu wengine wanaohitaji mikopo wanakaribishwa kuomba mkopo, kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kuongeza nguvu kazi ya taifa.
Mh. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Elias Masumbuko, akizungumza katika hafla hiyo.
Masumbuko amebainisha hayo akieleza kuwa lengo la Manispaa ni kukuza ustawi wa maendeleo kwa makundi yote kujiongezea kipato.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha, amevitaja vikundi vilivyopatiwa mkopo kuwa ni YOSE, Marida, Hisa Mageuzi, Princess, Ushonaji B (Wanawake), Nguvu Kazi, Waendesha Bodaboda Kata ya Mjini, Waendesha Bodaboda Bushola na Kikundi cha Wezesha Maisha kutoka kata ya Chamaguha.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga