- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Jumla ya Miradi nane (08) yenye thamani ya Tsh. 1,344,653,360 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 11.05.2019. Miradi hii inajumuisha ya Halmashauri (Tsh.39,020,260), Serikali kuu (Tsh.310,472,100), Sekta Binafsi (Tsh.750,000,000) na mchango wa wadau (Tsh.245,161,000). Ukiwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwenge wa Uhuru umekimbizwa umbali wa kilometa 102.5, katika Kata ya Kizumbi (Miradi miwili), kata ya Masekelo (Mradi mmoja), kata ya Mwawaza (Mradi mmoja), kata ya Ibadakuli (Miradi miwili) na kata ya Mjini (Miradi miwili), kuzindua na kuona miradi mbali mbali.
Aidha miradi hiyo iliyozinduliwa na kuonwa na Mwenge ni:
Miradi yote iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ilikubalika kwa asilimia 100 na kufunguliwa.
Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa leo tarehe 12.05.2019 katika wilaya ya Kishapu.
Tazama picha za matukio ya Mwenge hapa chini
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akiwa na kamati yake ya Mwenge wakiusubiri Mwenge wa Uhuru kutoka Halmashauri ya Msalala
Mkuu wa Wilaya ya Kahama akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa wilaya ya Shinyanga katika Manispaa ya Shinyanga
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akiwa amebeba Mwenge wa Uhuru
Mchungaji akiwakabidhi wakimbiza Mwenge pamoja na watu wote mikononi mwa Mungu kwa sala fupi ili zoezi lifanyike kwa amani
Sheikh wa wilaya akiomba dua njema katika kuukaribisha Mwenge wa Uhuru
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akikagua mradi wa ufugaji wa samaki katika moja ya mabwawa katika mradi huo
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akipanda mti aina ya Royal Palm katika kuunga juhudi za uhifadhi wa mazingira
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ufugaji wa samaki na uhifadhi wa mazingira ktk kata
ya Kizumbi kijiji cha Nhelegani
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akiwasikiliza kwa makini kikundi cha vijana kinachokemea rushwa ya ngono VETA Shinyanga
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akisikiliza ripoti kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Mafuta GILITU PETROLEUM STATION
Jiwe la msingi lililosimikwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ktk Kituo cha Mafuta GILITU PETROLEUM STATION
Mmoja wa watumbuizaji katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Shinyanga
Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Shinyanga akitoa ripoti ya Mradi wa Vyumba vitano vya madarasa katika s/m Viwandani
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akiweka jiwe la msingi katika S/m Viwandani baada ya kuridhishwa na mradi
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akikagua mradi wa Tarafa ya Ibadakuli
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akitoa sifa kemkem katika mradi wa Jengo la Tarafa ya Ibadakuli
Mradi wa maji
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akiweka jiwe la msingi katika mradi wa maji
Mganga Mkuu wa Manispaa akitoa ripoti ya Mradi wa uboreshaji Zahanati ya Mwawaza kwa kujenga jengo jipya la maabara
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akikagua jengo la maabara katika Zahanati ya Mwawaza
Kamishna wa Polisi akitoa ripoti ya Mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Polisi
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akifungua kwa kuweka jiwe la msingi Mradi wa Nyumba za Askari Polisi
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akiwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Uhuru
Mradi wa pikipiki
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akionyeshwa document za pikipiki katika mradi wa kikundi cha vijana wamiliki na waendeshaji
wa pikipiki maarufu kama bodaboda
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akikagua mabanda yaliyokuwa na shughuli mbalimbali ktk uwanja wa Sabasaba
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga (kushoto) akikaribishwa na mwenyeji wake Mkuu wa wilaya ya Kishapu alipokwenda kukabidhi Mwenge
wa Uhuru baada ya zoezi la kukagua miradi katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kumalizika.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga