- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MIRADI YA MANISPAA YA SHINYANGA YAPITA KWA KISHINDO
Na.Shinyanga Mc
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga umepitisha Miradi ya Maendeleo kwa kishindo huku kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Abdalla Shaib Kaim amewataka wananchi kutunza na kuitumia Miradi hiyo vizuri ili kuendelea kupata fursa ya kupewa miradi mingi zaidi kwa ajili ya maendeleo ya wana Shinyanga.
Hayo ameyasema leo alipokuwa akikagua, kuzindua, kufungua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi ya maendeleo 10 yenye jumla ya thamani ya bilioni 2,078,473,124.40
Pamoja na kazi hizo kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ndg. Abdalla Shaibu amefurahishwa na namna ya utekelezaji wa Miradi iliofanya kwa kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha iliyotumika.
Mwenge wa Uhuru 2023 katika Manispaa ya shinyanga imeweka jiwe la Msingi miradi (2),imekagua Miradi (3), kuzindua miradi (2), kufungua miradi (2) na kuona Mradi 1.
Pamoja na Mambo mengine Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa akiambatana na Timu ya wakimbiza Mwenge na viongozi mbalimbali wameshirikiana na wananchi kufanya usafi katika eneo la upendezeshaji liliopo Kalogo na kupanda miti katika shule ya sekondari Rajani ikiwa ni kielelezo cha kuunga mkono kauli mbio ya Mwenge huu wa uhuru inayosisitiza Utunzaji wa Mazingira na vyanzo vya Maji .
Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga umekimbizwa leo 28 Julai, 2023 umbali wa kilomita 72.5 na kesho 27 Julai, 2023 utakabidhiwa katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga