- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MKOA wa Shinyanga umekusanya zaidi ya shilingi Bilioni 255 kama mapato yatokanayo na shughuli za Madini, katika kipindi cha miaka miwili ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani.
Hayo yamebainishwa leo Machi 25, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mh. Christina Mndeme katika Kongamano la miaka miwili ya mafanikio ya Utawala wa Rais Samia lililofanyika leo Machi 25, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wakiwamo na Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga.
Mh. Mndeme ameeleza kuwa Makusanyo hayo yanahusisha ada za leseni, mrabaha na ada za ukaguzi zinazokusanywa kupitia Wizara ya Madini.
Ameeleza kuwa Mkoa wa Shinyanga umetoa leseni mbalimbali za madini 827 katika kipindi hicho cha miaka miwili.
Ameongeza kuwa vituo viwili vya ununuzi wa madini vimeanzishwa ikiwa ni mkakati wa kusogeza huduma za biashara ya madini karibu na maeneo ya wachimbaji wadogo.
Mndeme ametoa taarifa hiyo wakati wa kongamano la kuangazia mafanikio yaliyopatikana mkoani Shinyanga ndani ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika hatua nyingine, Mh. Mndeme amesema Mkoa wa Shinyanga umefanikiwa kujenga vyumba vipya vya madarasa 833, mabweni 3 na matundu ya vyoo 1,003 katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akielezea mafanikio ya miaka miwili ya Rais Samia.
Amesema “Mkoa umepokea zaidi ya shilingi Bilioni 37.68 katika sekta ya elimu na kufanikiwa pia kukarabati shule kongwe mbili za msingi”.
Amesema zaidi ya shilingi Bilioni 3.18 zimetumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 108, mabweni 3, matundu ya vyoo 1,002 na kukarabati shule kongwe mbili za msingi.
Amesema “shilingi Biliioni 20.32 zimetuika kujenga shule mpya 7, vyumba vya madarasa 725 kwa shule za sekondari, shilingi bilioni 11.96 zimetumika kugharamia elimu bila ada na shilingi bilioni 2.21 zimetumika katika ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Wilayani Kishapu”.
Aidha, katika Utawala wa miaka miwili ya Rais, Dkt. Samia, Mh. Mndeme amesema Mkoa wa Shinyanga umejenga viwanda vipya 108 katika kipindi cha miaka miwili kuanzia mwezi Machi mwaka 2021 hadi mwezi Februari mwaka huu na kuufanya kufikisha jumla ya viwanda 838.
Kabla ya kujengwa kwa viwanda hivyo vipya, mkoa huo ulikuwa na viwanda 730, lakini kutokana na fursa za uwekezaji zilizofunguliwa na Serikali ya awamu ya sita viwanda 108 zaidi vimejengwa katika mkoa huo ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.79.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akielezea mafanikio ya miaka miwili ya Rais Samia katika Wilaya ya Shinyanga.
Viwanda vingi ni vile vinavyoongeza thamani ya mazao ya kilimo na mifugo pamoja na uchimbaji wa madini ya dhahabu na almasi.
Mbali na Mh. Mdeme, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mh. Johari Samizi, amebainisha kuwa katika Utawala wa Miaka miwili ya Mama Samia, ndani ya Wilaya ya Shinyanga, Miradi ya Ujenzi wa Masoko ikiwemo Soko la Ibinzamata, Ngokolo Mtumbani na Soko Kuu inayotekelezwa na Mapato ya Ndani kutoka Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga inaendelea, halikadhalika Ujenzi wa Vituo vya Afya ikiwamo Ihapa na Kambarage ambayo Serikali imewezesha kujenga ili kuongeza ufanisi wa huduma.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga