- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu ameipongeza Manispaa ya Shinyanga katika utekelezaji wa miradi sekta ya afya hususani Hospitali ya Manispaa katika utoaji wa huduma kwa wananchi wote.
Pongezi hizo amezitoa leo tarehe 13 Julai, 2023 alipofanya ziara kwa lengo la kufuatilia utoaji wa huduma za kiafya , ujenzi wa miundominu , upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika Hospitali ya Manispaa. Ikumbukwe kwamba Mhe. Ummy Mwalimu aliagiza Wakurugenzi wote kuajiri watumishi wa mkataba kupitia mapato ya ndani ili kupunguza uhaba wa watumishi katika kada ya afya ambapo katika Hospitali ya Manispaa tayari walishaanza kutekeleza agizo hilo na Zaidi ya milioni 70 zimeshakwisha tengwa kwa ajili ya watumishi hao jambo ambalo Mhe. Ummy lilimfurahisha na kumpongeza Mkurugenzi na Manispaa kwa ujumla.
Aidha, kando na pongezi hizo Mhe. Ummy pia alifurahishwa na ujenzi wa jengo la dharula [EMD] Unaoendelea katika Hospitali ya Manispaa na kuwataka wataalam wa afya kutoka mikoa iliyoko pembezoni waje kujifunza namna bora ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa majengo ya dharula.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Ummy alipongeza pia huduma nzuri zinazotolewa katika Hospitali hiyo na kuwaomba watumishi wa Hospitali hiyo kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa kwa kuzingatia maadili ya kazi, miongozo,kanuni, taratibu za utoaji wa huduma za afya ,matumizi mazuri ya lugha kwa wagonjwa na kuwaomba waendelee kutoa huduma kwa upendo na utu.
Ikumbukwe kuwa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga awali ilitambulika kama Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinganga, lakini baada ya kujengwa Hospitali mpya ya mkoa Mwawaza, kwa sasa Hospitali hii ipo chini ya Manispaa ya Shinyanga na inatambulika kama Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga na imeanza kazi rasmi tarehe 01 Julai, 2023.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga