- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Diwani wa kata ya Ndala Mhe. Zamda Mwebea ameshinda uchaguzi wa naibu Meya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika baraza la Madiwani la mwaka uliofanyika leo tarehe 31 Julai, 2024 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za halmashuri ya Manispaa ikiwa ni awamu ya pili mfululizo (2023/2024-2024-2025.)
Awali akitoa ufafanuzi juu ya Mgombea nafasi ya Naibu Meya Mkuu wa Division ya Utawala na Usimamizi Rasilimali watu Manispaa ya Shinyanga Ndg. Pius Sayayi amesema Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ilipokea jina moja tu la Mgombea ngazi ya Naibu Meya wa Manispaa, hivyo kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi jina hilo litapigiwa kura za “Ndiyo” na “Hapana”.
Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo Mwenyekiti wa Uchaguzi ambaye pia ni katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Ndg. Said kitinga amesema Mhe. Zamda ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia zote.
“Jumla ya wapigakura ni 19, kura zilizopigwa ni 19, kura za hapana (0) kura zilizo haribika ni (0) kura za ndio ni (19), hivyo kwa mamlaka niliyopewa Mhe.Zamda Mwebea namtangaza kuwa ndiye Mshindi wa ngazi ya Naibu Meya manispaa ya Shinyanga” amesema Ndg. kitinga
Kwa upande wake Naibu Meya Mhe. Mwebea amewashukuru wajumbe kwa kumuamini tena na kumchagua nafasi hiyo kwa mwaka wa pili Mfululizo na kuahidi kuendelea kushirikiana ili kuleta maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga