- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MHE. MOHAMED MCHENGERWA AKABIDHI MAGARI YA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA SEKTA YA AFYA MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa leo tarehe 14 Novemba, 2023 amekabidhi Magari Manne ya usimamizi wa shughuli katika Sekta ya Afya ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa Waganga Wakuu wa wilaya na Mkoa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga.
akizungumza katika zoezi hili la kukabidhi Magari haya Mhe. Mchengerwa amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa na Waganga Wakuu wa Halmashauri, kuyatumia kikamilifu katika kuwatembelea Watumishi wa Afya pamoja na kufanya nao vikao vya mara kwa mara, ili kuboresha utendaji kazi wa kuhudumia wananchi na kuokoa Afya zao, wakiwamo wajawazito na kupunguza vifo vya uzazi.
"Nakabidhi Magari haya Manne ya usimamizi katika Mkoa wa Shinyanga ambapo gari moja ni la Mganga Mkuu wa Mkoa, na Mengine Matatu ni ya Waganga Wakuu wa wilaya, hivyo yatumieni Magari haya kwenda kufanya vikao na watumishi na kukagua huduma za afya ili wananchi wapate huduma bora za matibabu." amesema Mhe. Mchengerwa.
Awali, Mhe Mchengerwa alipata wasaa wa kuongea na Watumishi wa Sekta ya Afya na kuwataka kuendelea kutoa huduma stahiki za matibabu kwa wananchi, pamoja na kuhudumia Wajawazito ipasavyo na siyo kutanguliza pesa mbele, bali wawapatie huduma kwanza ili kumuokoa yeye na mtoto wake.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu kwa kuendelea kuboresha huduma za afya Mkoani humu, kwa kutoa fedha nyingi na kujengwa Vituo vya Afya, Zahanati,Hospitali za Wilaya, Mkoa, kutoa Vifaa tiba, Madawa, na sasa ameleta Magari Manne ya usimamizi kwa Waganga Wakuu.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga