- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MHE. KATAMBI AKABIDHI GARI LA WAGONJWA , VITANDA HOSPITALI YA MANISPAA YA SHINYANGA PAMOJA NA KUGAWA MAJIKO YA GESI.
Na. Shinyanga Mc
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu amekabidhi gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’ na Vitanda 8 kwa ajili ya wagonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na majiko 145 ya gesi kwa makundi mbalimbali ya jamii.
Akizungumza wakati wa kukabidhi gari, vitanda na majiko ya gesi leo tarehe 8 Februari, 2024 katika Stendi ya daladala ya Kambarage, Mhe. Katambi amesema gari hilo pamoja na vitanda vitasaidia wananchi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
“Nimekuja kukabidhi gari hili ‘Ambulance’ niliyopewa na Mama, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili lisaidie kuboresha huduma za afya katika hospitali yetu ya Manispaa ya Shinyanga. Pia baada ya kutoa vitanda 17 leo nimeamua kuongeza vitanda vingine 8 ili vikasaidie katika wodi zetu. Rais Samia anataka wananchi wapate huduma bora za afya”, amesema Mhe. Katambi.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Katambi amesema serikali inayoongozwa na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya afya, elimu, barabara na ujenzi wa masoko.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Ndg. Revocatus Lutunda amemshukuru Mhe. Katambi kwa kushughulikia haraka changamoto ya gari la wagonjwa pamoja na kuongezewa vitanda.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga