- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Shinyanga MC
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Johari Samizi, Februari 24, 2023 ameongoza Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kilichofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Shinyanga huku akiwataka Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji kwenda kuiweka LISHE kuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao na mikutano yao yote.
Amesema hayo ili kuhakikisha kuwa Wilaya ya Shinyanga inaondokana kabisa na matatizo yote yatokanayo na ukosefu wa LISHE likiwamo tatizo la UDUMAVU ni lazima sasa Watendaji waongeze juhudi katika kuelimisha umma juu ya madhara yatokano na kutozingatia kanuni za lishe na kwamba njia pekee oliuopo ni kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha kwa kushirikiana na wataalamu wa Lishe kutoka katika Halmashauri.
"Niwatake sasa Watendaji wote kwenda kutoa elimu ya kutosha kwa kushirikiana na wataalamu wa Lishe, mkatoe elimu hiyo katika kikao na mikutano yenu yote na kwamba suala la Lishe liwe ni ajenda ya kudumu kwenu," alisema Mhe. Johari.
Awali akimkaribisha kufungua kikao hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga Bi. Nice Munisi alisema kuwa wao kama Halmashauri ya Shinyanga pamoja na Halmashauri pacha ambayo ni Manispaa ya Shinyanga wanaendelea na juhudi za utekelezaji wa shughuli za Lishe kama ambavyo takwa la Serikali na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kinavyowaelekeza ili kwenda kuondoa kabisa tatizo kubwa la udumavu kwa watoto katika Halmashauri zote zilizopo Wilaya ya Shinyanga.
Kwa upande wao wataalamu kutoka Halmashauri ya Shinyanga na Manispaa walisema kuwa pamoja na kuendelea na utoaji wa elimu kwa umma lakini pia wameendelea na upimaji wa Chumvi ya Madini Joto, utapiamlo pamoja na vipimo vingine huku wakiwasisitiza wananchi kuepukana kabisa na imani ambazo zinawapeleka kwa waganga wa jadi ambako wamekuwa wakiaminishwa kuwa matatizo hayo ni ya kienyeji.
Akifunga kikao hicho, Mhe Johari aliwasisitiza na kuwakumbusha watendaji wote kwenda kusimamia suala la utoaji wa chakula mashuleni suala ambalo ni utekelezaji wa maahizo ya Serikali kuu, pia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda alisisitiza pia.
Mwisho aliwataka kwenda kuitafuta na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025 sambamba na maelekezo ya Serikali katika kutekeleza suala la Lishe ili kwenye kikao kijacho kila mtendaji atoe taatifa jinsi alivyotekeleza maagizo hayo.
Aidha alisema kuwa yeye Mhe. Johari kwa muda wake atachagua Shule yoyote na wakati wowote atakwenda kukagua utekelezaji wa Lishe kupitia Klabu za Lishe jambo ambalo alikwishalisema awali kuwa kila shule ihakikishe kuwa inayo Klabu ya Lishe.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga