- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh. Dkt. Yahaya Nawanda, Februari 10, 2023 amekabidhi Pikipiki 221 kwa ajili ya Maafisa Ugani katika Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi pikipiki hizo, Dkt. Nawanda aliwaeleza Maafisa Ugani hao pamoja na viongozi kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa, imedhamiria kwa dhati katika kuwawezesha wataalamu wa Serikali ili waweze kuongeza tija na ufanisi ulio bora zaidi kwa wananchi wanaowahudumia.
"Serikali hii inayo dhamira njema kabisa kwa wananchi wake, ndiyo maana sasa imeendelea kuwaboreshea mazingira kuwa bora ya utendaji kazi kwa watumishi ili waweze kuwahudumia kwa ufanisi zaidi wananchi wa Tanzania.
“Leo tupo hapa kuwapatia pikipiki hizi kama vitendea kazi ili kuwarahisishia katika utendaji kazi wenu" alisema, Mhe. Dkt. Nawanda.
Aidha, Dkt. Nawanda alitumia nafasi hiyo pia kuwatahadharisha maafisa ugani hao kuwa, wasiende kuzitumia tofauti Pikipiki hizo, kwakuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya maafisa ambao wamekuwa wakizitumia tofauti na kusudio lake jambo ambalo halikubaliki.
Katika hafla hiyo, Serikali imegawa jumla ya pikipiki 221 ambapo 82 zimetolewa kwa Wilaya ya Shinyanga, 39 Wilaya ya Kishapu na Wilaya ya Kahama wakipewa pikipiki 100.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga