- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Manispaa leo amefungua mafunzo ya mfumo wa kielektroniki wa uhasibu na utoaji taarifa unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS). Mfumo huu wa kielektroniki unasaidia utekelezaji wa utoaji wa rasilimali fedha moja kwa moja kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma kwa kuimarisha uhitaji wa kuwepo kwa usimamizi wa fedha katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma. "FFARS itawapatia nyie watoa huduma mfumo sanifu uliorahisishwa ambao utawawezesha kutunza taarifa za fedha zinazotolewa na zilizopo katika vituo vyenu. FFARS itaweza kufuatilia matumizi ya fedha hizo katika kufikia malengo ya utoaji huduma na kuhakikisha yanaendana na sheria za manunuzi na utoaji taarifa. Taarifa hizi zitasaidia Serikali kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma na kuongeza uwazi, na hivyo watoa huduma wa afya kuwa na wajibu kwa jamii wanayoihudumia.". Alisema Mkurugenzi wa Manispaa.
Kuanzia Julai 1, 2017 Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania iliaanza kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya kwa ngazi za Halmashauri. Vituo vya kutolea huduma ambavyo vinapokea fedha hizo vinajumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, na Hospitali za Wilaya. Zoezi hili ni sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta ya elimu, Serikali za Vijiji na Ofisi za Kata.
Wakufunzi wa mfumo wa FFARS na PlanRep kutoka Idara ya Afya, Fedha na Mipango (Ndugu Emmanuel, Divina Masali na Alex Mpasa) kutoka Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa
Mfumo huu mpya wa kupatiwa Rasilimali Fedha unatoa motisha kwa vituo vya kutolea huduma za afya na kuongeza kipaumbele cha utoaji huduma bora kwa wananchi wa Tanzania na kuongeza usawa na uwazi. Upelekaji wa Rasilimali Fedha moja kwa moja kwa vituo vya kutolea huduma inahakikisha kuwa Fedha zinazotolewa na Serikali zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa. Mkakati huu mpya wa kuboresha sekta ya afya ni msaada kutoka Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).
Mafunzo ya Mfumo wa FFARS yamekusudia kuwawezesha watumishi katika vituo vya Sekta ya Afya na Elimu kupata ujuzi wa namna ya kutumia mfumo wa kielektroniki wa FFARS ambao ndio watumiaji wa mwisho wa mfumo wa FFARS katika Vituo vya Afya, Zahanati na Shule za Msingi na Sekondari za Manispaa ya Shinyanga. Mafunzo haya yatahakikisha kuwa watoa huduma katika vituo wana ujuzi unaohitajika katika usimamizi wa fedha na kutoa huduma bora kwa wananchi wote Tanzania na kwa jamii zenye uhitaji.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo kutoka katika vituo vya kutolea huduma
Mfumo huu wa FFARS unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI); Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na USAID. Mfumo utatumika katika vituo vyote vya kutolea huduma ya afya na shule, na uhuishaji huu wa mfumo utarahisishia na kuongeza ufanisi katika mifumo ya Serikali ya Tanzania na kuboresha usimamizi na matumizi ya Rasilimali za umma.
Pamoja na mafunzo ya FFARS, pia watumishi watajifunza mfumo mpya na ulioboreshwa wa kupanga bajeti unaojulikana Planing and Reporting (PlanRep) ambao utaanza kutumika kuandaa bajeti ya Halmashauri kwa mwaka 2018/2019. Mfumo huu utapunguza gharama zilizokuwepo wakati wa uandaaji wa bajeti ya Halmashauri kama vile gharama za kutengeza vitabu vya bajeti, gharama za usafiri wa kupeleka bajeti katika ngazi ya mkoa na Wizarani. Kwa maana mfumo utaruhusu uandaaji wa bajeti na utumaji wa bajeti kielektroniki kutoka ngazi ya kutolea huduma hadi wizarani bila kuhitaji watumishi kusafiri.
Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni wa miaka mitano na unatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania bara. PS3 inafanya kazi katika sekta mbalimbali ili kuimarisha mifumo ya mawasiliano, utawala bora, fedha na rasilimali watu, hususani kwa jamii zenye uhitaji.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga