- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MEYA MANISPAA YA SHINYANGA AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI CHAZO CHA MAJI CHA MTO KIDALU
Na. Shinyanga Mc
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko ameongoza zoezi la upandaji Miti katika Chanzo cha Maji Mto Kidalu, ili kukitunza chanzo hicho pamoja utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Zoezi hilo la upandaji Miti limefanyika leo Disemba 27, 2023 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, pamoja na waandishi wa habari wakiongozwa na Mwenyekiti wao Ndg. Greyson Kakuru ambaye pia ni Mwandishi wa habari kutoka Shirika la utangazaji Tanzania TBC.
Akizungumza katika zoezi hili la upandaji mit Mhe. Masumbuko amelipongeza Shirika la utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuratibu upandaji huo miti na kushirikisha viongozi,huku akitoa wito kwa wananchi wa Shinyanga kuendelea kuzitumia mvua zinazoendelea kwa kupanda miti.
“Natoa wito kwa wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kuendelea kuzitumia mvua ambazo zinaendelea kunyesha kwa kupanda miti kwa wingi, ili kuyatunza mazingira na hata kuupendezesha Mji wetu wa Shinyanga na kuwa wa kijani,”amesema Mhe. Masumbuko.
Naye Afisa Maliasili na Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. Ezra Manjerenga ametoa wito kwa wananchi wa Shinyanga kuendelea kupanda miti kwa wingi ya matunda na kivuli, na wale ambao wanahitaji miti wanaweza kufika katika Ofisi yake ili wapewe miti bure.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoani Shinyanga Ndg. Greyson Kakuru, ambaye pia ni Mwandishi wa habari (TBC)amewashukuru viongozi pamoja na wananchi, kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hili la upandaji miti.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga