- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na. Shinyanga Mc
Manejimenti ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikiongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya shinyanga Ndg. Charles Luchagula ambaye ni mkuu wa kitengo cha Utamaduni Sanaaa na Michezo leo tarehe 7 Januari, 2025 imefanya ziara ya kukagu na kutembelea miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga.
Menejimenti imefanya ziara hiyo ya kukagua na kutembelea miradi ya maendelea kwa lengo la kuangalia ni hatua gani ujenzi umefikia katika miradi hii huku menejimenti ikiwataka wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ili majengo yaanze kutumika.
“ Niwatake muongeze kasi ya ujenzi kwa kila hatua mliyofikia ili majengo yaanze kutumika kwa wakati ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki ukizingatia Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani amekwisha toa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu mbalimbali katika sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu.” Amesema Ndg. Charles Luchagula
Miradi ya Maendeleo ambayo Menejimenti imeweza kutembelea na kukagua ni Ujenzi wa mabweni 4 shule ya sekondari Rajani, Ujenzi wa Sekondari mpya katika kata ya Kizumbi, ujenzi wa nyumba za Walimu katika shule ya sekondari butengwa, ujenzi wa madara 3 shule ya msingi ndala B.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga