- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya shinyanga Mwl. Alexius Kagunze amewataka watendaji wa kata, mitaa, madereva, watunza kumbukumbu,watumishi kada ya afya pamoja na waandishi wa vikao ajira mpya kuwa na nidhamu, kuzingatia maadili ya kazi
kuheshimiana na kushirikiana katika utendaji kazi ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Mwl. Kagunze ameyasema haya leo Januari 15,2024 wakati akifungua mafunzo kwa watumishi wapya walioajiriwa katika kada mbalimbali kwenye utumishi wa umma, mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo na uelewa kwa watumishi hao, mafunzo yaliyofanyaka katika Ukumbi wa mikutano shule ya msingi Buhangija.
“Ninyi ni watu wa muhimu sana katika ujenzi wa taifa mnatakiwa kufanya kazi yenu kwa bidi , kuzingatia maadili ya kazi, kutekeleza majukumu yenu, wajibu wenu ni kuwatumikia kikamilifu wananchi , rai yangu kwenu tufanye kazi kwa kuheshimiana na kushirikiana, tuwe na nidhamu kazini, mimi nikiwa ndiye Mkurugenzi wa Manispaa hii sitopenda watumishi wangu wanagombana, mkubwa amheshimu mdogo na mdogo vile vile amuheshimu mkubwa”. Amesema Mwl Kagunze.
katika hatua nyingine Mwl. Kagunze amewataka watumishi hao kutunza mali na rasilimali za serikali ili viweze kudumu.
“Watumishii wote watendaji wa mtaa ,kata, madereva hakikishenu mnatunza mali za serikali na kuzithamini. Serikali imefanya kazi kubwa sana katika Manispaa yetu ya Shinyanga Kuhakikisha inaweka vifaa na miundombinu rafiki ya utendaji kazi, nitumie fursa hii kuwaasa tuvitunze vifaa hivyo ili viweze kudumu”. Amesema Mwl. Kagunze.
Katika Mwaka wa fedha 2024/2025 halmashauri ya manispaa ya shinyanga imeweza kuajiri jumla ya watumishi 73, ambapo kada ya afya watumishi 44, madereva 3, watunza kumbukumbu 5 na watendaji 4, mitaa 16 , idara ya ujenzi mtumishi 1, pamoja na waandishi wa vikao 1.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga