- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya shinyanga Mwl. Alexius Kagunze ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari iliyopo kata ya kizumbi, hii ikiwa ni baada ya kumvunjia mkataba wa awali mkandarasi ambae ujenzi wa mradi huo ulikua ukisuasua.
Mwl. Kagunze ameridhishwa na kasi ya ujenzi hiyo leo Machi 05, 2025 baada ya kufanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi huo wa shule ikiwa ni miongoni mwa miradi ya elimu inayoendelea kutekelezwa ndani ya manispaa ya shinyanga.
“Mradi huu hapo awali ulikuwa ukisuasua kutokana na kasi ya mkandarasi aliyekuwepo, lakini kwa kasi hii aliyonayo mkandarasi mpya mradi huu utakamilika haraka ili kupunguza umbali wa kutembea kwa wanafunzi waishio maeneo jirani na mradi huu, hizi zikiwa ni jitihada za dhati za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata elimu katika mazingira yanayo fikika kwa wepesi”. Amesema Mwl. Kagunze
John Maige na Pili Juma ni baadhi ya wakazi wa maeneo hayo ambao wameishukuru Serikali kwa kutambua changamoto waliyokuwa wakipitia Watoto wao kwa kutembea umbali wa kilometa 8 kutafuta elimu hali ambayo ilikuwa ikiwafanya Watoto wengi kushinda kufikia ndoto zao ikiwa ni pamoja na kukumbana na wanyama wakali akawimo fisi pamoja na kushindwa kuwahi muda wa masomo.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga