- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze leo aprili 03, 2025 amefungua mafunzo ya sensa ya Elimu Msingi kwa walimu wakuu kwa shule za msingi, maafisa Elimu Kata, Mafunzo yanayolenga kuwajengea uelewa wa namna ya ujazaji wa dodoso ya Idadi ya walimu katika shule husika, taarifa za uthibiti bora wa shule, miundombinu, vifaa muhimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, taarifa za fedha, Maambukizi ya VVU pamoja na mapango wa shule salama.
Akifungua mafunzo haya yaliyojumuisha walimu wakuu wa Shule za msingi za serikali na shule binafsi ,maafisa elimu kata, walimu watakwimu wa shule na maafisa elimu takwimu ngazi ya msingi manispaa ya shinyanga kwenye mafunzo yaliyofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa na kuwataka walimu hao kujaza taarifa kwa usahihi, kwa wepesi ili serikali iweze kuweka mikakativya mamna ya kuongeza wigo wa ufundishaji wanafunzi katika mazingira rafiki na salama kulingana na mahitaji ya wanafunzi.
“Twendeni tukahuishe taarifa hizi kwa wepesi, usahihi na kwa ufasaha serikali ipate taarifa hizi na kuweka mipango mikakati kwa wepesi kwa sababu sisi hapa Manispaa ya Shinyanga tupo mjini hakuna chagamoto ya mtandao ni matumaini yangu ndani ya siku tatu hadi nne taarifa hizo zitakuwa zimekamilika”. Amesema Mwl.Kagunze
Katika hatua Nyingine Mwl. Kagunze amempongeza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lubaga Mwl. Stella L. Halimoja kwa kufanya vizuri Katika mitihani ya darasa la saba kwa Mwaka wa masomo 2024 ambapo shule hiyo imeshika nafasi ya kwanza kwa ngazi ya wilaya huku ikishika nafasi ya tatu kwa ngazi ya mkoa ambapo wanafunzi wamefaulu kwa daraja “A” na “B” ambapo jumla ya wanafunzi 60 walipata daraja “A” na wanafunzi watano pekee wakipata daraja “B” kwa Jumla ya ufaulu wa 100%
Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi Msingi Manispaa ya Shinyanga Mwl. Merry Maka amewasihi walimu hao kufanya kazi kwa kushirikiana ili kufikia kiwango Cha ufaulu wa asilimia 95% ikiwa ni maadhimio yao kwa Mwaka huu wa Elimu.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga