- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na George Mganga, Shinyanga Manispaa
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Mh. Jasinta Mboneko amewataka Maafisa Maendeleo pamoja na Waratibu wa Elimu kuonesha ushirikiano mzuri katika utekelezaji mpango wa Afua za Lishe kwa watoto mashuleni.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mh. Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Lishe.
Hayo amezungumza leo katika kikao cha Kamati ya Lishe kilicholenga kupitia mkataba wa lishe kwa Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika katika Ukumbi wa Kalinjuna, Manispaa ya Shinyanga.
Mboneko ametoa msisitizo huo akieleza kuwa kumekuwa na changamoto nyingi kwa watoto waliopo mashuleni, hivyo kupelekea kuwaagiza Maafisa kuonesha ushirikiano ili kuhakikisha watoto wanapata chakula ili kuepukana na changamoto za kiafya.
“Nasisitiza, Maafisa Maendeleo, Waratibu wa Elimu, wote tuoneshe ushirikiano kuhakikisha suala la lishe linazingatiwa mashuleni.
“Mpeane ushirikiano mzuri ili watoto waweze kupata chakula. Kuanzia Januari kwa shule za msingi na sekondari waanze kupata chakula”, amesema.
Aidha, kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, John Tesha, amebainisha kwa kueleza wapo tayari kuonesha ushirikiano ili kufikia lengo.
John Tesha, Afisa Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akizungumza
Tesha ameeleza hayo huku akiwataka wahusika wote kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii hususani kuyazingatia yaliyosemwa na Mkuu wa Wilaya pamoja na yaliyojadiliwa kwenye kikao huku akisisitiza kutolewa zaidi kwa elimu.
“Sisi tuko tayari kutoa ushirikiano kwa yote tuliyozungumza leo, tutaoa elimu ili kuongeza uelewa zaidi kuhusiana na masuala ya shule hususani katika Kata za Chibe, Ndala na Old Shinyanga”, amesema Tesha.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga