- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga idara ya afya ikiongozwa na mganga mkuu wa Manispaa imetoa elimu ya ugonjwa unaoenea kwa kasi zaidi duniani wa CORONA-Covid 19 kwa watumishi wa Manispaa leo asubuhi tarehe 21/04/2020.
Mganga mkuu ameelezea tahadhari zinazotakiwa kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji yanayochuruzika,kuvaa barakoa na kuzibadilisha kila baada ya masaa matatu,kupunguza mikusanyiko isiyo ya lazima.
Pia ametoa mifano ya namna ya kuvaa barakoa kwa usahihi,na aina ya barakoa ambazo zinatakiwa kununuliwa ambapo alipendekeza ‘Surgical Mask’ kuwa ni bora zaidi na zinazuia virusi kwa zaidi ya asilimia 90 (90%)
Vilevile Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga amesisitiza watumishi kuchukua hatua Madhubuti za kujikinga wenyewe ili kuwakinga wanaowazunguka.
Aidha Ofisi ya Manispaa ya Shinyanga imechukua hatua ya kujikinga na ugonjwa wa CORONA kwa kuweka ndoo za kunawia pamoja na sabuni nje na ndani ya ofisi za Manispaa. Pia kila idara imepewa ‘Hand Sanitizer’ kwa ajili ya matumizi ndani ya ofisi.
Kutokana na hatari ya virusi hivi, Halmashauri ya Manispaa inahakikisha kila mtu anaeingia ndani anapimwa joto kwa kutumia kifaa maalum.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga