- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na. Shinyanga MC
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imepongezwa kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo mpaka kufikia Aprili, 2023 Manispaa imekusanya zaidi ya Bilioni 5 sawa na asilimia 108 dhidi ya lengo la asilimia 100 iliyokadiriwa.
Pongezi hizo zimetolewa leo terhe 4 Mei, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi alipokuwa akitoa salamu za Serikali katika Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika katika Ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanya.
"Nichukue fulsa hii kuwapongeza sana Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ukiongozwa na Mstahiki Meya Mhe. Elias Masumbuko kwa upande wa Madiwani na Ndg. Jomaary Satura kwa upande wa Menejimenti na watumishi wote wa Manispaa kwa namna ambavyo mnafanya kazi kwa umoja, juhudi, maarifa na ubunifu mkubwa katika kukusanya mapato ya Serikali hadi kufikia Aprili 2023 tayari mmevuka lengo la mwaka, hongereni sana kwa hatua hii", alisema Mhe. Johari.
Pamoja na pongezi hizo lakini Mhe. Johari alisisitiza zaidi katika ubunifu, bidii na nidhamu ya fedha za Serikali na katika uongezaji wa vyanzo vya mapato ili kuongeza wigo wa ukusanyaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo iweze kutekeleze kwa kasi zaidi jambo ambalo litawaletea maendeleo wananchi ambao ndiyo wenye miradi na fedha zao.
Aidha alikumbusha juu ya umuhimu wa kutunza mazingira, vyanzo vya maji na usafi kwa ujumla kwakuwa Tanzania kama Nchi inajumuika na nyingine katika kupambana na masuala ya Tabia Nchi jambo ambalo ni Ajenda ya dunia kwa sasa. Huku akiwaeleza kuwa kuna ujio wa Mwenge wa Uhuru ambao unayo Kauli Mbiu inayosisitiza utunzaji wa mazingira na kwa Manispaa Mwenge utapokelewa tarehe 28 Julai, 2023.
Awali Ndg.Mensaria Mrema (Afisa Mipango) akisoma taarifa ya utekelezaji kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa alisema kwa kipindi cha robo ya 3, 2023 Manispaa imepokea Tzs. 1, 715, 900,000/ ikiwa ni fedha za bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Elimu na ujenzi wa nyumba za viongozi.
Picha ikimuonesha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga (aliyesiama) akitoa ufafanuzi wa jamho wakati mkutano wa Baraza la Madiwani Mei 4, 2023 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliyopo Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. Jomaary Mrisho Satura akimkaribisha Mstahiki Meya kwa ajili Itifaki ya Mkuu wa Wilaya mapema leo katika mkutano wa Madiwani.
Muonekano wa baadhi ya waheshimiwa madiwani kaika picha ya ukumbini kahla ya kuanza kwa mkutano.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga