- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Baraza la Madiwani, wakuu wa vitengo na idara pamoja na watumishi wa halmashauri ya manispaa ya shinyanga wamefanya ziara Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani katavi kwa lengo la kujifunza namna ya Kuendesha na kuzalisha biashara ya Gesi joto (Kaboni) inayozalishwa katika vijiji nane vilivyopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani katavi.
Ziara hiyo imefanyka Disemba 30, 2024 Katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ambapo wamejifunza namna ya uendezeshaji wa mradi wa hewa ya ukaa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi inayosababishwa na Shughuli za binadamu, pamoja na kutembelea bandari ya Kalema iliyopo ziwa Tanganyika.
Awali akizungumza Mwezeshaji ambaye pia ni Afisa Misitu Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Ndg. Ephrahim Luhwago amesema moja ya jambo la kuzingatia kufanya biashara hii lazima Kijiji kiwe kimesajiliwa na kiwe na cheti ya Ardhi, pia Kijiji hicho kiwe na msitu kuanzia Nusu hekari.
“Kwetu sisi Tanganyika tunafanya uzalishaji wa hewa ya ukaa Katika maeneo ya Misitu na maeneo ya malisho ya mifugo, halmashauri tulibuni mradi wa uzalishaji wa hewa ukaa ili kuweza kuwanufaisha wakazi wa Kijiji husika, kwa mfano kwa Kijiji Cha Kagunga mradi huu wa hewa ukaa kwa Mwaka 2024, tumezalisha jumla ya Bilion 1.3 ambayo imetumika kujenga huduma za kijamii Katika Kijiji hiki ikiwepo zahanati ya kagugu, kurekebisha miundombinu ya barabara pamoja na kuajili watumishi wa sekta ya afya watano kutokana na mapato hayo”. Amesema Ndg. Luhwago.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko kuniaba ya Madiwani na Manejimenti ya Manispaa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa kubuni miradi ambayo inanufaisha moja kwa moja wakazi wa Kijiji husika, huku akiwashauri kuongeza umakini wa usimamizi wa mapato yanayo patikana ili yaweze kutumika kwa Shughuli husika kama yalivyo malengo ya Halmashauri.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga