- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Imetoa Jumla ya Kiasi cha Milioni Mia Moja Laki Nane Sabini na Tano Elfu(100,875,000) kwa Vikundi Sita vya Wajasiriamali ikiwa ni Maelekezo ya Serikali kutenga Asilimia 10 ya Mapato ya Ndani kwa Ajili ya Mikopo kwa Vikundi vya Akina Mama,Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Akiongea Mgeni Rasmi wa Zoezi hilo la utoaji Mikopo kwa vikundi vya Ujasiriamali Rev:Dr(Phd) Kulwa Ezekiel Meshack Ambaye ni Mwenyekiti wa TCCIA Shinyanga ,"Nawasihi na kuwaomba Mkopo huu mkautumie kwa Kuendesha shughuli za kujikuza kwenye shughuli zenu za Kijasiriamali kama ambavyo vile Tumekubaliana kwenye dhima ya Mkopo huu,Tutangulize Nidhamu na kujitoa kwenye kutimiza Malengo ya Mkopo huu lakini tusisahau Kufikiri lengo na Dhumuni kuu la Mikopo hii"
Naye Mstahiki Meya wa Halmashauri Mh Elias Ramadhani Aliwapongeza Timu mzima ya Manispaa Mkurugenzi na Wasaidizi wake kwa hatua hii na Kutimiza Dhima ya Serikali kwa kutoa mikopo kwa Vijana, Akina Mama na Watu wenye Walemavu, Aidha kwa upande Mwingine Mstahiki Meya Aliwaasa Wanavikundi hao Kurejesha Mkopo huo kwa Wakati kwa Maana Pia kuna Wengine wana Uhitaji na Mikopo hiyo ili kujikwamua kwenye shughuli zao za Ujasiriamali.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga