- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na George Mganga, SHY MC
HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga imetoa mafunzo ya matumizi ya Vishikwambi kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari ili kurahisisha utendaji kazi kwa Wanafunzi pia kuendana na mfumo wa Kidijitali.
Mafunzo hayo yaliyotolewa January 30, 2023 katika Ukumbi wa Nkonoki uliopo Shule ya Savannah Plains mjini Shinyanga, yalihusisha pia Maafisa Elimu Kata halikadhalika Maafisa Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari na yaliendeshwa na Mwezeshaji Ndg. Anthony Gikuri Nchangwa, kutoka Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi, Shinyanga, ambayo ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Manispaa ya Shinyanga imeamua kutoa mafunzo hayo ili kusaidia Walimu kuendana na mfumo wa TEHAMA ikiwemo usahihishaji wa mitihani, ambao utawezesha kupata data mbalimbali kupitia mtandao.
Ikumbukwe Novemba 4, 2022, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Ugawaji wa Vishikwambi 293,400 kwa Walimu wote nchini, alisema lengo ni kuboresha mazingira ya ufundishaji kwa njia ya TEHAMA, huku akiagiza vishikwambi hivyo kuwafikia walengwa pasipo ubadhilifu na kuwasisitiza Walimu kuvitumia kwa matumizi sahihi.
Katika utekelezaji wa agizo la Mh. Majaliwa juu ya kugawa Vishikwambi kwa Walimu wote, tayari Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imetekeleza zoezi la ugawaji wa Vishikwambi vyote 1019 ambavyo vilitumwa kutoka Serikalini.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga