- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imetoa mafunzo kwa wafanyabiashara jinsi ya kuweza kutumia mfumo wa TAUSI katika shughuli zao ili kuwapunguzia usumbufu wa kwenda Ofisi za biashara kupata huduma hiyo.
Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo, Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bi. Naely Nasomi alisema kuwa, Serikali imeanzisha mfumo mpya ambapo Mfanyabiashara sasa ataweza kujihudumia yeye mwenyewe kwa kuomba kupitia Link ya Tausi.tamisemi.go.tz bila kupata usumbufu wa kwenda kwa Afisa Biashara ambapo atapata Control Number itakayomuwezesha kulipia na kupata Leseni.
Katika mafunzo hayo wafanyabiashara walikubaliana kwa kauli moja kwenda kuutumia mfumo huo huku wakiahidi kuwasaidia na wengine ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo ambayo yalitolewa bure gharama yoyote.
"Sisi hatuna tatizo na Manispaa yetu, lakini tunaomba kupitia Halmashauri kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wafanyabiashara kwa wingi wetu kwani mfumo huu ni mpya, na wengi hawaufahamu na hivyo ili kuepuka misuguano isiyokuwa na ulazima kati ya Serikali na sisi wafanyabiashara," alisikika mmoja wa wafanyabiashara akisema.
Akifunga mafunzo hayo Mwenyekiti wa muda aliyeteuliwa na wafanyabiashara hao ambaye pia ni Diwani Kata ya Ngokolo Mhe. Victor Nkwizu alisema kuwa, wafanyabiashara hawana tatizo na Serikali kwakuwa mrejesho utokanao na Kodi wanazolipa unaonekana katika miradi mikubwa ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga.
"Wakishirikishwa huwa hawana shida kabisa, kikuwa ni ushirikishwaji kwa kila kitu hasa mambo yanayohusu malipo kwa Serikali na kwamba linapotokea jambo jipya kama hivi na tukashirikishwa sisi hatuna neno tutatekeleza makubaliano haya boal shida," alisema Mhe. Victor
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia vikao vyake vya ndani iliadhimia kwa kauli moja kuwaita wafanyabiashara ili kuwapatia mafunzo hayo ya mfumo mpya wa TAUSI ili ikasaidie katika kuomba, kupata Control Number na hatimae mfanyabiashara akilipia ataipata Leseni yake kupitia mtandao na wala hakuna ulazima wa kufika ofisi za biashara kwa ajili ya jamno hilo.
Mfumo huu wa TAUSI unatajwa kuwa mwarubaini wa kukomesha rushwa, urasimu na hata upotezaji wa muda katika upatikanaji wa Leseni kwa wafanyabiashara jambo ambalo litaongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga