- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MANISPAA YA SHINYANGA YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
Na. Shinyanga Mc
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imepongezwa kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa.
Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 25 Septemba, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokagua ujenzi wa jengo la dharula (EMD) katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na kuweka Jiwe la Msingi, Upanuzi wa miundombinu katika Shule ya Sekondari Old Shinyanga na kuweka Jiwe la Msingi pamoja na Zahanati ya Seseko ambapo aliweka Jiwe la ufunguzi.
"Niwapongeze wananchi, Viongozi na Watumishi kwa ujumla kwa kutekeleza vizuri usimamizi wa miradi ya maendeleo hakika mmejua kuthamini thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali niwaombe miradi yote tuitunze vizuri ili tuendeleee kupokea miradi mingi zaidi " alisema Mhe. Mndeme
Pamoja na pongezi hizi lakini Mhe. Mndeme amewasisitizia wahudumu wa afya kutumia lugha nzuri wanapohudumia wagonjwa pamoja na kupunguza matumizi ya simu yasiyo ya lazima wanapohudumia wagonjwa.
Aidha, Mhe. Mndeme alipata wasaa wa kuongea na wananchi wa Seseko kata ya Mwamalili kwa kusikiliza kero zao ambapo waliwasilisha kero ikiwemo ukosefu wa umeme na utokaji wa maji kwa siku chache,
Changamoto hizi ziliweza kujibiwa na wataalamu husika na Mhe. Mndeme kuwataka Wataalamu hao mpaka ifikapo tarehe 30 Novemba, 2023 umeme uwe umeshafika katika kata ya Mwamalili na kwa upande wa maji idara ya Shuwasa imepewa mwezi mmoja na nusu ili tatizo la utokaji wa maji kwa siku chache uwe umeisha na badala yake maji yawe yanatoka kila siku.
Sanjali na hayo, Mhe Mndeme amewataka wananchi wa Seseko kutoa taarifa za ukatili pale zinapotokea na sio kukaa kimya, kuendelea kupanda miti na sio kuikata pamoja na kuendelea kuwapatia chakula wanafunzi wanapokuwa shuleni ili kuendelea kuongeza Kasi ya ufaulu.
Ziara hii ya Mhe. Mndeme ni mwendelezo wa ziara zake kwa lengo la kutembelea, kukagua na kufanya mikutano ya hadhara kwaajili ya kusikiliza kero za Wananchi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga