- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MANISPAA YA SHINYANGA YAPONGEZWA KWA USHINDI WA USAFI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Na. Jesca Kipingu -SHY MC
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo tarehe 10 Agosti, 2023 imepongezwa na Baraza la Madiwani kwa ushindi wa usafi na utunzaji wa mazingira iliyoshindanishwa na Halmashauri nyengine 5 katika Mkoa wa Shinyanga.
Akiwasilisha taarifa ya ushindi huo mbele ya Waheshimiwa Madiwani Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze ameeleza kuwa Halmashauri 5 zimeweza kushindanishwa katika swala la usafi na utunzaji wa mazingira ambapo Manispaa ya Shinyanga imeibuka mshindi wa kwanza na kupatiwa tuzo, cheti na vifaa vya kuhifadhia uchafu zikiwemo taka hatarishi na zisizo hatarishi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme jana katika kikao cha Tathimini ya Lishe Mkoa.
"Tumeibuka washindi kati ya Halmashauri 5 tulizo shindanishwa nazo kwa kuzingatia vigezo tulivyowekewa vya ushindani tulivifikia na sasa tumeibuka washindi " alisema Mwl. Kagunze
Awali Mwl. Kagunze alisema Serikali ya Mkoa iliweka vigezo kadhaa vya kuzipima Halmashauri vikiwemo uwepo wa dampo la kisasa, upendezeshaji wa mji, usafi wa mazingira kwenye mitaa na vijiji, ujenzi wa vyoo kwenye masoko na stendi za mabasi pamoja na usafi wa mazingira kwenye mitaro ambapo kwa Manispaa vigezo hivyo vyote walikuwa navyo na kuibuka mshindi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga