- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeshinda tuzo mbili baada ya kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa kwa ngazi ya Mkoa ambapo kwa ufaulu wa jumla katika mtihani wa kidato cha nne (SCEE) jumla ya ufaulu wa 97.34% huku kwa mtihani wa kuhitimu darasa la saba (PSLE) imeshinda kwa jumla ya ufaulu wa 88.42% kwa mwaka wa masomo 2024.
Akikabidhi Tuzo hizi leo Aprili 04,2025 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha katika kikao kazi cha tathimini ya elimu kilichowakutanisha wadau wa elimu kutoka Halmashauri tatu, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga iliyopo ndani ya Manispaa ya Shinyanga , Mhe. Macha ametumia fursa hiyo kuipongeza Manispaa ya Shinyanga kwa kufanya vizuri kwenye mitihani hiyo huku akitoa wito kwa walimu wote mkoani Shinyanga kuongeza mbinu za ufundishaji ikiwa ni pamoja na kuandaa mitihani ya mara kwa mara ili kuwasaidia wanafunzi kuwa na uzoefu wa kujibu mitihani na kuwasaidia kufikia ndoto zao.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetekeleza majukumu yake kwa 100% swala la matokeo mazuri na ufaulu kwa mwanafunzi ni wetu sisi wadau wa Elimu, hususani walimu, inasikitisha sana Mtoto anasoma mazingira mazuri, bora na salama tena bila ada harafu anafeli hii kwa mkoa wa Shinyanga haikubaliki, Wito wangu kwa walimu wa shule zote za Msingi na sekondari twendeni tukasimamie ufaulu kwa wanafunzi, kitu pekee kwa walimu kujivunia ni kuona wanafunzi wametimiza ndoto zao kupitia uwekezaji huu wa serikali”. amesema Mhe. Macha
Katika hatua nyingine RC Macha amepiga marufuku kwa shule binafsi mkoa wa Shinyanga zinazowapima wanafunzi wao kupitia mitihani yao ya ndani na kuwafanya wanafunzi hao kurudia darasa ambapo amesema mtihani pekee unaowapima wanafunzi ni unaotolewa na Serikali kwa kuzingatia maksi zilizowekwa na Serikali.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga